NJOO WEWE NA YULE KATIKA ‘SKYLIGHT SUNDAY BONANZA’‬ KIOTA CHA ESCAPE ONE LEO JIONI


Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akiwasebenesha sehemu ya mashabiki wao sambamba na Sony Masamba jumapili iliyopita kwenye Skylight Sunday Bonanza‬ kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam na hivi leo mwendo ni ule ule na speed 120.(Picha na Geofrey Adroph wa pamoja blog).
Rapa Joniko Flower akichuana na mmoja wa shabiki wa Skylight Band staili mbalimbali za sebene huku mashabiki wengine wakiangalia na kuiga miondoko hiyo.
Msanii Em Evans kutoka bendi ya Wana Njenje akijumuika kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band jumapili iliyopita kwenye kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar...Kwa mbali ni Tophy Bass akicharaza nyuzi kisawa sawa.
Msanii Em Evans kutoka bendi ya Wana Njenje sambamba na Kasongo Junior wa Skylight Band katika kolabo matata sana kuonyesha kipaji chao, njoo leo uwashuhudie Live kiota cha Escape One Mikocheni.
Em Evans na Kasongo Junior wakiendelea kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi kutoka Skylight Band, Joniko Flower katika hisia kali kuwapa raha mashabiki wake kiota cha Escape One, Mikocheni jumapili iliyopita ambapo leo pia mwendo ni ule ule, bila kukosa njoo wewe na yule waambie na wengine pia bila kukosa katika fukwe tulivu kabisa.
Kasongo Junior katika hisia kali sambamba na Joniko Flower kwenye kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar.
Kasongo Junior na Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita, bila kukosa ya leo itakuwa pale pale.
Bamutu wa Congo wakiburudisha mashabiki wa Skylight Band Joniko Flower na Sony Masamba ni ndani ya kioata cha Escape One Mikocheni jijini Dar.
Sam Mapenzi akiongoza marapa wenzake wa Skylight Band, Sony Masamba na Joniko Flower kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.
Shabiki mzalendo wa Skylight Band, Miryam Kamaliza (kushoto) akipata Ukodak na shasti yake wa karibu ndani ya kiota cha Escape One.
Raia wa Asia kwa mbali wakionekana kuchiziki na Skylight Band...mpaka chini hiyo hapana chezea kabisa.
 
Sony Masamba akichana mistari kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku Joniko Flower, Sam Mapenzi na Kasongo Junior wakimsikindiza kwa miondoko ya aina yake.
Mashabiki wakiendelea kujimwaga na burudani ya Skylight Band kiota cha Escape One.
Joniko Flower akichana mistari huku Sony Masamba akiwafundisha mashabiki wa Skylight Band moja ya staili Jumapili iliyopita kwenye kiota cha Escape One.
Mashabiki wakiendelea kusebeneka na burudani ya Skylight Band.
Sony Masamba na Sam Mapenzi wakiwapigisha kwata mashabiki wa Skylight Band jumapili iliyopita kwenye kiota cha Escape One pale Mikocheni kabla ya daraja la Kawe....usikose leo pia kwenye lile Skylight Bonanza.
Kutoka kushoto ni Joniko Flower, Sony Masamba, Suzy na Sam Mapenzi wakitoa burudani kwa mashabiki wao (hawapo pichani kwenye kiota cha Escape One Jumapili iliyopita.
Mashabiki wakitweta jasho na sebene la Skylight Band.
Rapa mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akiwapa burudani sehemu ya mashabiki wa band hiyo.
Hapo sasa twende kazi.....
DSC_0645
Pale mashabiki wa Skylight Band wanapowazidi kingi waimbaji kwa kucheza staili zao na mwishowe inakua hivi....inaitwa copy and paste.....ni mashabiki wazalendo wa Skylight Band.
Hapa sasa ni mwendo wa kusebeneka tu.
Mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga na lisebene.
Sony Masamba akiwapa shangwe mashabiki wa Skyight Band.
Sam Mapenzi akichana mistari huku mmoja wa mashabiki akijitahidi kusebeneka 'style' flani Amazing'
Sam Mapenzi na Joniko Flower wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
Mdau Mulle na mabinti wa Skylight Band wakisebeneka kwenye dancing floor.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment