RAIS MAGUFULI AMTEUA DK TULIA ACKSON KUWA MBUNGE

Aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Tulia Ackson Mwansasu.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, leo asubuhi ametengua uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu, Dk Tulia Ackson Mwansasu na kumteua kuwa Mbunge.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene, ameithibitisha kutenguliwa na kuteuliwa kwa Dk Tulia.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Thomas Kashilila amekiri kupokea taarifa ya uteuzi wa Dk Tulia mapema leo asubuhi.
Awali kabla ya uteuzi huo, Dr Tulia alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini pia, jana Novemba 15, 2015 aliteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment