UKATILI WA KIJINSIA SOKO LA TEMEKE WAPUNGUA KWA ASILIMIA 70

 Mwezeshaji  Sheria katika Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam  leo, kuhusu mafanikio waliyopata ya kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya kupatiwa mafunzo na Shirika la Equality for Growth (EfG). Kushoto ni Mwezeshaji wa Sheria, Christina Simon na Augenia Gwamakombe.
 Mkuu wa Mgambo katika soko hilo, Onesmo Osward (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Mfanyabiashara wa matunda katika soko hilo, Isabela Juakali akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Augenia Gwamakombe (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Mfanyabiashara wa Soko hilo, Said, Mbonde (kulia), akizungumzia kupungua kwa ukatili wa Kijinsia katika soko hilo.
Wanawake wafanyabiashara katika soko hilo wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

UKATILI wa kijinsia katika Soko la Temeke umepungua kwa asilimia 70 ukilinganisha na miaka mitatu iliyopo imefahamika.

Hayo yalibainishwa na Mwezeshaji wa Sheria wa soko hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika soko hilo, Christina Simon wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea soko hilo Dar es Salaam leo asubuhi kujua changamoto za ukatili wa jinsia katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth kutoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na ukatili huo.

"Hivi sasa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko letu umepungua kwa kiasi kikubwa baada ya wanawake kujitanbua na kupatiwa mafunzi na shirika la EfG" alisema Simon.


Alisema awali matukio ya unyanyasi kila wiki walikuwa wakiyapokea kati ya matatu na zaidi lakini sasa kwa mwezi wanaweza kupokea tukio moja au lisiwepo kabisa.

Mwezeshaji wa Sheria, Taus Ali,  alisema katika soko hilo kulikuwa na unyanyasaji mwingi, lugha za matusi ambazo likuwa zimekithiri lakini hivi sasa hali hiyo haipo na kama ipo ni kwa kiwango kidogo hasa baada ya kuletewa mradi wa Mpe Riziki si Matusi na EfG.

Mfanyabiashara, Said Mbonde alisema hivi sasa unyanyasaji wa kijinsia kwenye soko hilo haupo kwani hapo awali kulikuwa na tabaka la kufanyabiashara kwani biashara aliyokuwa wanaifanya wanaume walikuwa hawaruhusiw kufanya wanawake lakini sasa kila mmoja wao anafanyabiashara hizo zikiwemo za udalali.

Mfanyabiashara wa matunda katika soko hilo, Isabela Juakali alisema tabia iliyokuwepo zamani ya mgambo kuwamwagia biashara zao wafanyabiashara ndogo ndogo hivi sasa haipo kabisa baada ya kuelewa na kufuata kanuni na maelezkezo ya utendaji kazi.

Mkuu wa Mgambo katika soko hilo, Onesmo Osward alisema siku hizi malalamiko ya mtu kutukanwa au kupigwa hayapo kabisa jambo lililoongeza utulivu na amani katika soko hilo.


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment