VIDEO FUPI YA EVELINA MOCEVICIUTE- Alivyowafagilia Watanzania na Tabia zao za Kiungwana

Na Freddy Macha http://www.youtube.com/watch?v=rtp8_5Jw1KE Ulikuwa na wenzio Tanzania kwa miezi sita...Mbeya vijijini. Ulikaa na wananchi. Vipi ulijisikaje katika eneo hili la Afrika? "...Lilikuwa jambo la kipekee. Ilitupa changamoto na utofauti mkubwa, ambao sin’tokwawia kulirudia tena.
Kama nilivyokueleza awali kila siku tuliyokuwa vijijini ilikuwa kama wadhifa fulani. Maana tulitaka kuwa sehemu mahsusi ya jumuiya...wenyeji walitukaribisha, walituhusisha katika mambo yao...tulikaa na familia zao, tunashukuru sana kwa hilo. Walifungua milango yao. Wakatukaribisha. Mara nyingi ilibidi kujifinya, na kujiuliza je kweli, Mungu wangu niko kweli Afrika? Na hisia hiyo ya kutoamini maastajabu haikunitoka kwa miezi yote sita niliyokuwa Tanzania! Ni uzoefu ulionibadili sana. Nadhani wanavijiji wengi walikuwa na wasiwasi kwamba sisi Wazungu tulikuwa wasafi au tungeshindwa kuishi maisha yao. Ilibidi wahimizwe kuwa hakuna noma yeyote..." 10-Evelina na wenzake wakiwa na timu ya wanafunzi vijijini- Picha ya Evelina Moceviciute 2015 
  Evelina na wenzake wakiwa na timu ya wanafunzi Watanzania vijijini - Picha ya Evelina 


Moceviciute 2015 Wanafunzi wanavijiji Lukata na Evelina na wenzake Wanafunzi wanavijiji Lukata na Wageni waliowafundisha taaluma ya biashara. Picha ya Evelina Moceviciute https://youtu.be/rtp8_5Jw1KE
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.