“ALL THINGS AFRICAN” WALIVYOLIPAMBA SHOO LAKE LADY JAYDEE, LONDON

All Things African-2Si wengi wanaifahamu All Things African. Kampuni hii ndogo ya wanawake Uingereza imeanza kujenga jina kutokana rangi zake zenye bendera ya Tanzania na wanawake wachapa kazi wanaoongozwa na Hamida Mbaga. Jumamosi tarehe 5 Desemba 2015, All Things African, iliyapamba mazingira ya maonesho yake mwanamuziki Lady JayDee alipotumbuiza holi la Oasis, kitongoji cha Barking , mashariki ya London. Maonesho hayo yalitayarishwa na Upendo Events. Ushirikiano wa makampuni haya mawili unadhihirisha dira njema ya kazi na biashara baina ya Watanzania ughaibuni. Hali kadhalika wakati wa karamu ya kusheherekea miaka 40 kati ya Tanzania na Uingereza (British Tanzania Society) All Things African ilikuwa na meza yenye bidhaa mbalimbali za Kitanzania na Afrika mjini Reading

1- All things African - models and Admn- pic by F Macha 2015

Warembo, wafanyakazi, wasanii na wapambaji wa “All Things African” wakijivunia bendera ya Tanzania, kimavazi.

5- Bw  Frank Leo akiwa na mwimbaji Lady JayDee alipowasili London 2015
Muasisi wa Upendo Events, Bw Frank Leo akiwa na Lady JayDee mara alipowasili London, juma lililopita.
Picha ya Upendo Events
6- Lady JayDee jukwaani Oasis Club - Dec 2015- pic by F Macha

Lady JayDee akiwa jukwaa lenye mseto wa taa za rangi mbalimbali zilizompa wajihi wa kipekee, Oasis Bankqueting Suite.

Bw Frank Leo wa Upendo Events na mwimbaji na All Things African

Bw Frank Leo wa Upendo Events akiwa na msanii wa kizazi kipya toka Uganda, Hyper Hype. Nyuma ni Hamida Mbaga na Mjamaica, Thembi Watt, wote wa “All Things African.”
Wataalamu na wanasayansi  toka sehemu kadhaa za Uingereza walihudhuria tafrija. Hapa ni  Amri Dello (Mhandisi - umeme wa magari moshi), Catherine Eliezerly (Madini) na Riziki Lukanza (Madini).  Wataalamu na wanasayansi toka sehemu kadhaa za Uingereza walihudhuria tafrija. Toka kushoto Amri Dello (Mhandisi – umeme wa magari moshi), Catherine Eliezerly (Madini) na Riziki Lukanza (Madini).
10-Angel Newell akiyafurahia mavazi- pic by F Macha
Angel Newell, mwenye uzawa wa Nigeria na Jamaica, akiifurahia kazi yake ya sanaa ya mavazi ya “All Things African.”


Jasmine Kissamo Assenga- wa All Things African
Jasmine Kissamo Assenga akinadi lubega la Kimasai. Jasmine ni mshoni, msanifu mavazi, msusi, mpamba wajihi na sura na mmoja wa waendeshaji wakuu wa All Things African
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment