DKT. MAGUFULI MAALIM SEIF WATETA IKULU, NI KUFUATIA "MKWAMO" WA KISIASA VISIWANI ZANZIBAR

Maalim Seif Sharif Hamad na Rais John Pombe Magufuli wakifuanya mazungumuzo kuhusiana na hali ya kisiasa Zanzibar, mazungumuzo yaliyomhusisha makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani). Mauzngumumuzo hayo yalifanyika leo Jumatatu Desemba 21, 2015 Ikulu Dar es Salaam.
Maalim Seif Sharif Hamad na Rais John Pombe Magufuli wakielekea kuongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mazungumuzo kuhusiana na hali ya kisiasa Zanzibar, mazungumuzo yaliyochukua saa mbili Ikulu jijini Dar.
Rais John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mazungumuzo kuhusiana na hali ya kisiasa Zanzibar, mazungumuzo yaliyochukua saa mbili Ikulu jijini Dar.
Maalim Seif Sharif Hanad akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mazungumuzo kuhusiana na hali ya kisiasa Zanzibar, mazungumuzo yaliyochukua saa mbili Ikulu jijini Dar.
Angalia Video hapo chini.......


Na K-Vis Media
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani, leo Desemba 21, 2015 pale Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam, , amekutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia alikuwa Mgombea kiti cha Rais wa visiwa hivyo, Maalim Seif Sharif Hamad na kufanya nae mazungumzo.
Kwa mujibu wa maafisa wa Chama Cha Upoinzani CUF, ambacho Maalim Seif ndiye Katibu Mkuu wake, mazunhumzo hao yalidumu kwa muda wa masaa mawili (2), ambapo Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan pia alihudhuria.
Mazungumzo hayo yanakuja huku kukiwa na “mkwamo” wa kisiasa visiwani humo baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, kuufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25, 2015 akisema ulijaa mizengwe na kadhia nyingi na kwamba tume itapanga tarehe nyingine ya uchaguzi.
Hata hivyo tangazo hilo lilipingwa kwa nguvu nyingi na maafisa wa CUF akiwemo Maalim Seif mwenyewe huku akisisitiza kuwa yeye ndiye msindi halali na kwamba mwenyekiti wa tume hiyo hana mamlaka ya kikatiba kufuta uchaguzi huo.
Baada ya mkwamo huo wa kisiasa kumekuwepo na juhudi mbalimbali za viongozi wa juu wakiwemo viongozi wa dini, kufanya vikao vya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo ambapo hata Rasi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein, amekwisha kutana mara kadhaa na Maalim Seif ingawa hakuna taarifa zozote zililokwishatolewa na viongozi hao wawili juu ya nini hasa walichokuwa wakizungumza ingawa wafuatiliaji wa mambo wamekuwa wakibashiri kuwa ni juu ya mkwamo huo wa kisiasa.
Mkutano huo wa Dkt. Magufuli na Maalim Seif unaelezwa kuwa ndio mkutano mkubwa na muhimu zaidi hadi sasa na kwamba suluhisho la mzozo huo sasa majawabu yako “jirani”. Baada ya mazungumzo yao, wakitumia diplomasia, waliwaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo yalikuwa mazuri na kwamba wote wawili wanaimani suala hilo litamalizika haraka
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment