WAFANYAKAZI WA KITUO CHA MAFUTA CHA PUMA CHA UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM WATEKELEZA AGIZO LA RAIS KWA KUFANYA USAFI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mafuta cha Puma cha  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Brown Francis akishiriki kufanya usafi katika kituo hicho ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk.John Magufuli kuwa maadhimisho ya Siku ya Uhuru 2015 yatumike kwa kufanya usafi nchini kote.
 Meneja wa Kituo hicho, Shadrack Mwamaso naye akishiriki kufanya usafi.
 Hapa usafi ukiendelea.
 Hapa ni kazi usafi ukifanyika.
Ni kama anaongea 'Ngoja nikazitupe taka taka hizi eneo husika".
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mafuta cha Puma cha  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Brown Francis (kushoto), akiwaelekeza jambo wafanyakazi wenzake wakati wakifanya usafi katika kituo hicho.
 Hapa ni usafi tu kwa kwenda mbele.
 
Hapa ni bega kwa bega katika kufanya usafi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mafuta cha Puma cha  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Brown Francis akiwa sanjari na wafanyakazi wenzake wakati wa kufanya usafi.

 Wafanyakazi wa kituo hicho wakifanya usafi. Kushoto ni Ali Hussein na Charles Nkwera (kulia)
Takataka zilipelekwa eneo husika.

Na Dotto Mwaibale


WAFANYAKAZI wa Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wameungana na watanzania nchini kote kufanya ufasi ikiwa ni utekelezsaji wa agizo la Rais Dk.John Pombe Magufuli la kuitumia siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania 2015 kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.


Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Brown Francis alisema wamejisikia furaha kubwa kutekeleza agizo la Rais kwa kufanya usafi katika eneo lao la kazi.


"Tulijipanga na wafanyakazi wenzangu katika kutekeleza jambo ili ambapo ni muhimu kwa taifa letu la kufanya usafi wa mazingira na litakuwa ni endelevu" alisema Francis.


Francis alisema ni muhimu kwa kila mtanzania kujenga tabia ya kufanya usafi mara kwa mara katika maeneo yao badala ya kusubiri kuhimizwa na viongozi.


(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment