ZADIA yajiandaa na Maandamano Un NYC

Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA) inapenda kuwaarifu Wazanzibari, Watanzania na Wapenda Amani wote ulimwenguni kuhudhuria katika maandamano ya kushinikiza kumaliza mchakato wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika huko nyumbani Zanzibar tarehe 25/10/2015.
Maandamano hayo yatafanyika siku ya Ijumaa tarehe 18/12/2015 kwenye viunga vya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York kuanzia saa nne asubuhi (10:00 AM) hadi saa sita mchana (12:00 PM). Kufika kwenu kwa wingi na kwa wakati ndio mafanikio ya maandamano yetu haya.
Yoyote atakaesikia taarifa hizi anaombwa amuarifu mweziwe.
Asanteni
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment