Global yatoa mifuko 100 ya saruji ujenzi sekondari Kinondoni

4DC, Makonda (kulia) akipokea mfuko wa saruji kutoka wawakilishi wa Global, Elvan Stambuli (katikati) na David Mwaipaja (kushoto).
1Wanahabari wakichukua tukio katika hafla hiyo.
7Mifuko ya saruji ikiwa ndani ya gari la Global kabla ya makabidhiano.
6Elvan Stambuli (katikati) akionesha risiti ya makabidhiano hayo kutoka kwa Makonda (kulia), anayeshuhudia kushoto ni Ofisa Masoko wa Global, David Mwaipaja. 5. Mkuu wa Wilaya, Makonda (kulia), akionekana kutumia nguvu kubeba saruji wakati wa makabidhiano hayo. 8Mwakilishi wa Osyter Bay Pharmacy, Kefa Kijo (kulia) akimkabidhi saruji Makonda.
2Mwakilishi wa Global, Mhariri Mwandamizi, Elvan Stambuli, akihojiwa na wanahabari mara baada ya makabidhiano hayo.
3.DC, Makonda (kulia) akipokea mfuko wa saruji kutoka wawakilishi wa Global, Elvan Stambuli na David Mwaipaja.
KAMPUNI ya Global Publishers Ltd inayozalisha magazeti ya Championi, Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda, mapema leo imechangia mifuko 100 ya saruji katika ujenzi wa shule za sekondari wilayani Kinondoni, Dar. Mifuko hiyo imekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, na mwakilishi mwandamizi wa Global, Elvan Stambuli, katika ofisi yake iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam. “Nikiwa mwakilishi kutoka Global Publishers, ninakabidhi mifuko 100 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa sekondari kwa Wilaya ya Kinondoni kutokana na kuguswa na wito wa mkuu wa wilaya hii alioutoa kwa makampuni na taasisi mbalimbali kusaidia kuongeza shule saba za sekondari wilayani Kinondoni ili vijana waweze kupata elimu vizuri,’’ alisema Stambuli.   Wakati huohuo, naye mwakilishi kutoka kampuni ya Ubapa Limited, Wenceslaus Rwezahula, na mwakilishi wa Oyster Bay Pharmacy, Kefa Kijo, walitoa mifuko ya saruji kuchangia ujenzi huo. Hata hivyo mara baada ya makabidhiano hayo, Makonda aliishukuru Kampuni ya Global Publishers kwa kuchangia mifuko 100 akisema ni mfano wa kuigwa kwa makampuni mengine, huku akisisitiza kuwa bado taasisi na makampuni mengine yanayo fursa ya kuendelea kuchangia ujenzi huo.
PICHA/HABARI: DENIS MTIMA/GPL
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment