Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud Awafariji Wananchi Waliounguliwa na Nyumba yao Mtaa wa Kiponda Mji Mkongwe Zanzibar


Wananchi wakiangalia moja ya Nyumba katika Mtaa wa Kiponda ilioungua kwa moto usiku wa jana saa 1.30 na kuteketeza vifaa vyote vya wakaazi wa jengo hilo, katika ajali hiyo hakuna Mtu aliyejeruhiwa na Wakaazi wote waliwahi kutoka salama kunusuru maisha yao. kwa mujibu wa mashuhuda wa janga hilo wameseme moto huo umeazika katika sehemu ya juu ya jengo hilo kutokana na hitilafu ya umeme. 
Nyumba hiyo inaisha familia tatu. na zote zimetoka salama bila ya madhara yoyote. 
Baadhi ya vitu vilivyowahi kuokolewa katika nyumba hiyo.
Sehemu ya chini ya nyumba hiyo eneo hili ni la ngazi ya jengo hilo ambayo imeonguka wakati wa jitihada za kuuzima moto huo. 
Nyumba ya jirani na jengo hilo ambayo imeungua sehemu ya paa ya jengo hilo 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud akiwasili katika eneo hilo la tukio na kuwafariji Wananchi waliopata ajali hiyo ya moto. 
Mmoja wa Mkaazi nyumba hiyo Mzee Amini Ahmeid Ali akiwa na familia yake wakiangalia athari hiyo ya moto baada ya kuzimwa na Kikosi cha Zima Moto Zanzibar kwea kushirikiana na Wananchi wa Mtaa huo.
Mhe Mohammed Aboud akiwa katika moja ya chumba cha nyumba hiyo kilichoteketea kwa moto bila kupata vifaa viliokuweko humo ndani akiwa na familia ya Mzee Amini Ahmeid.
Baadhi ya Wana familia waliopata janga hilo wakiwa nje ya nyumba hiyo wakifarijiwa na Ndugu na Jamaa. kwa mkasa huo wa kuugunguliwa na moto.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud akiwafariji Wananchi waliopata ajali ya kuunguliwa na moto nyumba yao wakati alipofika kuwafariji kwa mkasa huo. na kuwataka kuwa wastaamilivu na kusubiri kupatiwa msaada kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar.


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment