MWENYEKITI WA CCM, KIKWETE AOMBA WAZEE KUUNGA MKONO UONGOZI WA RAIS MAGUFULI

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akilakiwa na  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo, kaba ya kukutana na kuzungumza na wazee wa Singida Mjini. Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Mary Maziku.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisubiri kuvalishwa skafu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo. Kushoto ni Mama Salma Kikwete. na Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Singida Mary Maziku na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
 Chipukizi wakimvalisha Skafu Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akienda katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, akiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete, Nape na Mary Maziku
 Kikwete akijadiliana jambo na Nape
 JK akiwasalimia wananchi
 JK akizungumza baada ya kupatiwa taarifa ya CCM Mkoa wa Singida. Kushoto ni Mary Maziku Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida
 Kina mama wakitumbuiza kwa ngoma kumlaki Kikwete Ofisi ya CCM mkoa wa Singida
 JK akisalimiana na mmoja wa wanachama wa CCM 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akionyesha jengo lililokuwa Ofisi ya TANU mkoa wa Singida miaka ya 75 akiwa katibu msaidizi wa TANU wa wilaya


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipiga picha na mke wake Mama Salma Kikwete, leo, mbele ya nyumba ambamoishi  mjii Singida mwaka 1975, wakati huo akiwa katibu Msaidizi wa  TANU  wilaya ya Singida mjini. Kikwete yupo mkoani Singida kwa ajili ya kuongoza Maadhimisho ya Miaka 39 ya CCM, abayo kilele chake kitaifa ni kesho

 JK akisalimiana na wazee alipowasili kuzungumza nao mjini Singida leo


Na Richard Mwaikenda,Singida

MWENYEKITI  CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amewaomba wazee kote nchini, kumuunga mkono Rais John Magufuli katika uongozi wake ili kumpa
moyo wa  kuwatumikia Watanzania.


Alisema, kipindi ambacho Dk Magufuli ameingia madarakani hadi sasa ni mda mfupi, hivyo si vema kuanza kudodosa na kulaumu panapopwaya, badala yake Wazee na watanzania kwa jumla wazidi kumuunga mkono ili kumtia moyo wa kutekeleza  yote aliyokusudia kuyafanya kwa manufaa ya taifa.Kikwete alitoa ombi hilo alipokuwa akizungumza katika mkutano na wazee wa Mkoa wa Singida, ambapo alisema kuwa kuongoza bila ushauri wa wazee nchi inaweza kuyumba."Kuongoza nchi bila wazee mambo hayaendi vizuri na  ukikosa mzee kwenye jahazi wapiga makasia vijana wanaweza kuanza kuzozana na chombo kwenda mrama, lakini wakiwepo wazee watawaongoza vizuri  na chombo/ nchi kwenda  salama". Alisema Kikwete huku akishangilia na wazee.Si Kila mzee ni mwasisi wa chama, kila mwenye mvi na mwasisi, wengine wameingia kwenye chama wazee. Alisisitiza kwamba ukitaka nchi itulie kamata wazee, lakini ukiongoza nchi kwa kutumia vijana  pekee nchi inaweza kuyumba, na itafika mahali mtakosa mahali pa kushika. Alisema kuwa hata yeye kwa mara ya kwanza .alipokwenda kuomba ubunge jimboni kwake Bagamoyo, Pwani aliunda kamati ya wazee ambayo ilimsaidia sana.Wazee ni sehemu ya matumaini ya chama na Serikali, panapokuwepo  wazee hapaharibiki jambo. "Nawashukuru sana wazee endeleeni kukijenga chama na kuiunga mkono Serikali inayoongozwa sasa na Dk John Magufuli." Alisisitiza Kikwete na kuongeza kuwa,"Hata kwenye chama chetu tumeunda Baraza la Washauri la Wazee wasitaafu, ambapo wengi walipinga, hata hao wazee tuliowataka waunde baadhi yao walipinga, lakini mwisho walikubali kwa masharti kwamba wawe wanaitwa panapotokea jambo kubwa litakalohitaji ushauri wao."Alisema mmoja wa viongozi aliyekuwa msitari wa mbele kuunda baraza hilo, alikuwa Rais msitaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye alitoa ushauri wa kuitwa kutoa ushauri panapotokea jambo kubwa na kwamba hata wakitoa ushauri, viongozi waliopo madarakani wawe hiari kuukubali au kuukataa'.Aliwataka wazee kuendelea kuiunga mkono serikali ya sasa ambayo kwa hivi sasa imetimiza muda mfupi wa miezi mitatu ambaye ni sawa na mtoto mdogo anayekua.
Alisema kuwa Jambo kubwa ni kuwaunga mkono, kuliko kuwalaumu ama sivyo watavunjika moyo, ndani ya miaka mitano itakuwa hasara. watieni moyo ili wajiamini wahudumie vizuri zaidi ili nchi isonge mbele kimaendeleo.Kikwete alisisitiza kuwa hata yeye akitakiwa kwenda kutoa ushauri atakwenda, na akiwa na jambo la kushauri atakwenda pia, lakini aliwaasa kuwa  si kila jambo wazee watake kwenda kutoa ushauri, itachelewesha mambo mengi.


JK akisalimiana na wazee alipowasili kwenye mkutano ambapo alizungumza na wazee wa mkoa wa Singida

 JK akiwasili katika mkutano na wazee wa Mkoa wa Sindida leo
 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungmza kabla ya kumkaribisha Mke wa Mwenyekiti wa CCM, Salma Kikwete kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Singida
 Mama Salama Kikwete akizungumza katika mkutano huo
 Katibu wa Baraza la Wazee Mkoa wa Singida,Athuman Sima akisoma risala mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Singida, Juma Mudida akiapa mbele ya Jakaya Kikwete kuwa yupo tayari kupambana na mtu yeyote alatayepingana na utumbuaji wa majipu unaofanywa na Rais Magufuli
 Jakaya Kikwete akizungumza katika mkutano na wazee amabapo amewaomba kuunga mkono uongozi wa  Rais John Magufuli ili nchi isonge mbele kimaendeleo.
 JK akiagana na mmoja wa wazee baada kumaliza kuzungumza nao
 JK akiagana na wazee baada ya kumaliza mkutano


Baadhi ya wazee wakiondoka baada ya kuzungumza na JK mjini Singida leo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment