RAIS DKT. JOHN MAGUFULI ASEMA "NIMEJITOA SADAKA KWA AJILI YA KUWATETE MASIKINI" AAPA KUENDELEA KUTUMBUA MAJIPU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt. John PombeMagufuli, akitoa hotuba wakati akiongeana wazee wa jiji la Dar es Salaam, kwenye ukumbiwa Diamond Jubilee, Jumamosi Februari
Rais John Magufuli akiwapungia wazee wa Dar es salaam kabla ya kuzungumza nao kwenye ukmbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Februari 13, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mke wa Rais, Janet Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wazee wa Dar es salaam kabla Rais John Magufuli hajazungumza nao kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Februari 13, 2016.
Rais John Magufuli akiteta na Waziri Mkuu, Kassim Majaliw katika Mkutano kati yake na wazee wa Dar es salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Februari 13, 2016
Rais akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (wapili kushoto), na Mwenyekiti wa Wazeew a Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Mkali (wapili kulia) wakishuhudia

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amesema yeye na wenzake serikalini wameamua kujitoa sadaka kwa ajili ya kuwatete masikini wa Tanzania.

Rais alitoa kauli hiyo wakati akihudtubia mamia yawazee wa jiji la Dar es Salaam, kwenye matangazo yaliyopeperushwa live na rininga hapa nchini, kutokea ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam Februari 13, 2016.

“Nitaendelea kutumbua majipu, kila yatakapojitokeza, iwe ni kwenye mkono, mguu, kichwani, mgongoni, kifuani, tumboni, nitatumbua tu mpaka yaishe na hali iwe nzuriyaTanzania na watanzania.” Alisema Mh. Rais huku akishangiliwa na wazee hao.

Rais alimaanisha kuwa, vitendo vya rushwa. Ufisadi na uhujumu uchumi ndivyo vilivyoifikisha Tanzania hapa ilipio ambapo, hakuna madawa ya kutosha, hakuna maji yauhakika, wanafunzi wanakaa chini.

Rais aliapa, kuwa mambo hayo lazima yawe historia kwani nchi inakila rasilimali inayowawezeshawatanzania kuishi maisha mazuri na kondokana na ile tabia ya kuomba.

Dkt. Magufuli ambaye alifuatana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majakliwa, na mkewe Mwalimu Janet Magufuli, aliwasihi watanzania kuwa wavumilivu na kuiunga mkono serikali yake wakati inachukua hatua hizo kali dhidi ya ubadhirifu wa mali ya umma.
Kuhusu mgogorowa kisiasa visiwani Zanzibar, Rais amesema kwamujibu wa Katiba ya Zanzibar, yeye hana mamlaka ya kuingilia masuala ya uchaguzi wa visiwani humo nakwamba mamlaka aliyonayo kama amiri jeshi mkuu ni kuhakikisha amani inatawala sehemu zote za Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania na kuonya, kuwa wale waliojipanga kuleta chokochoko watakumbana na mkono wa dola popote pale ndani ya Tanzania
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment