TFDA yateketeza bidhaa zilizokwisha muda wa kutumika Singida

Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kanda ya kati,imefanikiwa kukamata bidhaa mbalimbali zikiwemo vipodozi vilivyopigwa marufuku,vyakula,dawa na soda ambazo muda wake wa kutumika umekwisha, vikiwa na uzito wa tani 3.5 na thamani yake ni  zaidi ya shilingi Milini 13.8.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuteketeza kwa moto bidhaa hizo juzi, Mkaguzi TFDA kanda ya kati, Aberl Deule,alisema kuwa bidhaa hizo zimekamatwa kwenye maduka mbalimbali wakati wa ukaguzi uliofanyika kwa muda  wa siku 10.
“Ukaguzi huu ambao tumeufanya na maafisa kutoka Manispaa ya Singida, lengo lake ni kuhakikisha soko la bidhaa siku zote linakuwa na bidhaa bora ambazo hazina madhara ya aina yoyote kwa binadamu, “alisema Deule.
Deule ametumia fursa hiyo kuwataka/kuwaagiza wafanyabiashara wajenge utamaduni wa kujali afya za wateja na sio kutanguliza mbele maslahi yao binafsi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Singida, Dkt..John Mwombeki, alisema ofisi yake inafanya ukaguzi mara kwa mara kwenye maduka kwa lengo la kuhakikisha soko lina badhaa zinazofaa kwa matumizi ya kila siku ya binadamu.
“Wakati wa ukaguzi huo huwa pia tunawaelimisha wafanyabiashara kwamba sio vizuri kuwauzia wateja bidhaa mbovu ambazo ni hatari kwa afya zao,” alisema.
Katika hatua nyingine, Dkt. Mwombeki amewataka watumiaji wa pombe aina ya bia kuhakikisha kwanza wanakagua bia ili kubaini kama bado muda wake wa kutumiwa haujaisha ndiyo watumie.
“Watumiaji wengi wa bia huwa hawajali kukagua muda wa kutumika kwa bia kitendo kinachopelekea kunywa bia ambazo muda wake wa kutumika umekwisha au ina uchafu ndani yake,” alisema Mganga Mkuu.
Na Nathaniel Limu, Singida.
IMG_3144

Mkaguzi TFDA kanda ya kati, Aberl Deule, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya kukamata bidhaa ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu zenye uzito wa tani 3.5 na thamani yake ni shilingi 13.8 milioni. Bidhaa hizo ni pamoja na vipodozi vilivyopigwa marufuku, vyakula na soda ambazo muda wake wa kutumika umekwisha.

IMG_3132

Moto mkubwa ukiteketeza bidhaa ambazo muda wa kutumika umekwisha na vipodozi vilivyopigwa marufuku.

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment