JAJI MKUU WA ZANZIBAR AFANYA ZIARA PEMBA

JAJI mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (wa pili kulia) akifuatana na maafisa ya jeshi la Magereza Pemba wakati alipowatembelea mahabusu na wafungwa katika Gereza na Wete Pemba kufahamu matatizo mbali mbali yanayowakabili,
(Picha na Ameir Khalid).
AFISA wa kitengo cha komputa (IT) Mahakama za Pemba Mohamed Juma (kulia) akimfahamisha jambo Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, juu ya utendaji kazi wa komputa za Mahakama ya Wete wakati wa ziara yake Mahakamani hapo
AFISA Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji, Makaazi na Nishati Pemba Hemed Salum Hemed akizungumzia matatizo mbali mbali yanayoikabili Mahakama ya ardhi Wete, wakati wa ziara ya jaji mkuu katika Mahakama hiyo,
MKURUGENZI wa baraza na mji Wete Mgeni Othman aliyesimama akielezea matatizo mbali mbali yanayoikabili Mahakama ya Mwanzo Wete, wakati jaji mkuu wa Zanzibar alipofanya ziara Mahakamani hapo
MRAJISI wa Mahakama kuu Zanzibar Mhe. George Kazi (kulia) akichambua madudu mbali mbali yanaliofanywa katika Mahakama ya mwanzo Wete


JAJI Mkuu wa Zanzibar mhe. Omar Othman Makungu (katikati)akiangalia moja ya sehemu ya jengo la mahakama kuu Pemba iliyopo Chake chake baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa


MMOJA ya wazee wa Mahakama ya ardhi Chake chake Pemba Khamis Mzee akielezea matatizo mbali mbali yanayoikabili mahakama hiyo katika utendaji wake wa kazi za kila siku, wakati jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu alipofanya zaira katika mahakama hiyo
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment