MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AAPISHWA LEO

Balozi Seif Ali Iddi akipeana mkono wa hongera na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi kabla Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kumuapisha kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipeana mkono wa hongera Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid akiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (kushoto) wakati wa kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushika nafasi hiyo leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipitia hati ya kiapo kabla ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kumuapisha rasmi kushika nafasi hiyo aliyomteuwa,hafla ya kiapo ilifanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar(kushoto) Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
Washauri wa Rais wa Zanzibar wa mambo mbali mbali ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Mjini Unguja.
Balozi Seif Ali Iddi akielekea sehemu ya kula kiapo kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipoapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akibadilishana mawazo na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kumuapisha rasmi leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Mwanasheria Mkuu wa zanzibar Mhe,Said Hassan Said (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (katikati) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid wakiwa katika hafla ya kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushika nafasi hiyo leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto) akiwa na Viongozi waliohudhuria kuapishwa kwake leo,(wa pili kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mama Asha Suleiman Iddi baada ya kumuapisha Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar leo katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar,(Picha na Ikulu.]
Share on Google Plus

About JG Blog Team

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment