RAIS MAGUFULI AMKARIBISHA RAIS WA VIETNAM, MHE. TRUONG TAN SANG IKULU, DAR ES SALAAM

Msafara wa Rais wa Vietnam ukiwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016. 
 
(Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo)
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kulia) akiwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya ziara yake ya kikazi yenye kuendeleza mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam. 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akipokea ua toka kwa mtoto mara alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 akiwa ameambatana na mmewe kwa ajili ya ziara yake ya kikazi yenye kuendeleza mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia) akimkaribisha mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang mara alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye koti la drafti) mara alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016. Wa kwanza kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa tatu kushoto) mara alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia) pamoja na Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakipanda jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) pamoja na Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakiwa jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang(mwenye tai nyekundu) akikagua gwaride mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016. 
Umati wa watu wakiwa ndani Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang aliyewasili jana kwa ajili ya ziara yake ya kazi nchini Tanzania. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe mama
Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) wakiingia ndani ya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa mara ya kwanza kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye kukuza uhusiano baina ya Tanzania na Vietnam 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akisalimiana na akina mama waliompokea mara alipotembelea katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli (kulia) 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh pamoja na Mama Janeth Magufuli wakifurahia jambo 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akifurahia zawadi ya kinyago cha kuchonga alichokabidhiwa na mwenyeji wake mama Janeth Magufuli kama zawadi 9 Machi, 2016 katika ofisi za Mke wa Rais Jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akimpa zawadi mama Janeth Magufuli ikiwa shukurani yake mara alipotembelea katika ofisi yake 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake mama Mai Thi Hanh mara baada ya kutembelea katika ofisi hiyo leo 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akipata maelezo kuhusu nyaraka mbalimbali ziliko katika Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo 9 Machi, 2016. 
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment