WAJUMBE WATEULE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WAANZA KUFANYA USAJILI

Mjengo wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar lilioko katika mitaa ya Chukwani Zanzibar linategemea kuaza Vikao Vyake March 20, 2016 kwa Wawakilishi kula kiapo na Kuhutubiwa na Rais wa Zanzibar Dk Shein. 
Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Wawakilishi Chukwani ukiwasubiri Waheshimiwa kuapishwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein kulihutubia siku ya 30 March 2016 jioni.
Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akiwasili katika Jengo la Afisi ya Baraza la Wawakilishi chukwani kwa ajili ya Usajili wa matayarisho ya Wajumbe kuaza kwa Kikao cha Baraza baada ya kukamilika kwa Taratibu za kuwasajili Waheshimiwa Wawakilishi na kuapishwa na Spika.
Wawakilishi Wateuli wakiwasili katika Jengo la Afisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani Mwenye shati jeupe Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Ali Salum na Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji. 
Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Nassor Salim Jaziri akiwasili katika viwanja Jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kwa ajili ya Usajili leo asubuhi.
Wawakilishi Wateule Mhe Haroun Ali Suleiman na Mhe Ali Salum wakibadilisha mawazo na kupongezana kwa kurudi tena Mjengoni. 
Wawakilishi Wateule wa Majimbo ya Uzini na Kwamtipura Mhe Mohammed Raza na Mhe Hamza wakiwasila katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa Ajili ya Usajili, zoezi hilo limeaza leo kwa Wateule wote kwa ajili ya kuaza shughuli za Baraza baada ya kuapishwa.
Kwa hisani ya ZanziNews
Share on Google Plus

About JG Blog Team

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment