BWENI LA SEKONDARI YA ISENYE LATEKETEA KWA MOTO

Moto umeteketeza bweni la wasichana la Shule ya Sekondari ya Issenye na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh80 milioni na wanafunzi 43 kukosa malazi.
Tukio hilo, ambalo limeibua taharuki kubwa, lilitokea jana (Aprili 20) kati ya saa 5:00 na saa 6:00 mchana, ikiwa ni takriban miezi nane tangu wanafunzi wachome duka la shule hiyo julai mwaka jana wakipinga vitendo vya kunyanyaswa.
Mkuu wa shule hiyo, Joseph Nyamgonja aliiambia Mwananchi kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa kwa kuwa wanafunzi walikuwa darasani, lakini vitu vyote vya wanafunzi vimeteketea.
Alisema bado hawajajua chanzo cha moto kuibuka kwenye bweni hilo ambalo halina umeme.
"Nikiwa ofisini niliona wanafunzi wanakimbia kuelekea bwenini. Kutoka nje niliona moshi mkubwa kwenye bweni," alisema.
"Tulifanikiwa kubomoa mlango na kuokoa magodoro machache. Tulijitahidi kuzima kwa maji na mchanga, lakini hatukufanikiwa baada ya paa lote kushika moto," alisema.
Alisema vitanda 52 , magodoro na vitu vyote vya wanafunzi vimeteketea na tathimini ya awali inaonyesha kuwa moto huo umesababisha hasara ya zaidi ya Sh80 milioni.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment