GARI LATUMBUKIA BAHARINI ENEO LA FERRY JIJINI DAR ES SALAAM, WATU WAWILI WAHOFIA KUFARIKI

 
GARI aina ya Hiace limetumbukia baharini eneo la Ferry jijini Dar es Salaam mapema leo saakumi na moja alfajiri Aprili 20, 2016 na habari za mwanzo zinasema watu wawili mwanamke na mwanamme wanahofiwa kufa maji.
Mwili wa Mmoja wa watu hao ukitolewa mara baada ya kupatikana majini, juhudi za kuutafuta mwili mwingine zinaendelea.

Mashuhuda wanasema, wapiga mbizi kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi JWTZ, kikosi cha navy, wamefanikiwa kuokoa mwili wa mwanamume na kazi ya kutafuta maiti ya mwanamke inaendelea. 
Mashuhuda wanasema, Hiace hiyo ilitumbukia baharini kutoka kwenye kivuko (Ferry)  baada ya gari ilo kuvuka kwenye msitari wa magari yapotakiwa kuishia na ndipo gari likatumbukia na gari hilo bado hazijapatikana.Kwenye majira ya saa tatu waliweza kufanikisha kupata mwili wa mwanaume aliyekuwa kwenye hilo gari aian ya Hiace.
Boti ya mwendo kasi ya JWTZ, ikiwa na wazamiaji imeonekana eneo la pwani ya magogoni ikiwa kwenye kazi ya kutafuta gari pamoja na huyo mama aliyebakia kwenye gari hilo.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment