HATIMAYE mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania ( Bot), Amatus Liyumba, leo umeagwa katika nyumba yake iliyopo Mikocheni B, jijini Dar.
Akizungumza na GPL, mpwa wa marehemu, Arbogasti Chiwembo, alisema marehemu mjomba wake alifariki Aprili 18,
mwaka huu katika Hospitali ya Agha Khan kutokana na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu. Ameacha watoto saba na mwili wake utasafirishwa kesho alfajiri kuelekea Mahenge mkoani Morogogo kwa ajili ya mazishi.
Marehemu Liyumba aliwahi kukabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi kati ya mwaka 2001 na 2006 wakati wa ujenzi wa majengo pacha ya makao makuu ya BoT, ambapo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 221.
Habari :Gabriel Ng`osha na Denis Mtima/GPL
0 comments/maoni:
Post a Comment