UFAFANUZI JUU YA GOFUNDME AKAUNTI KWA JINA LA ANDREW SANGA*

Ndugu Wanajumuiya ,

Kuna akaunti ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia gharama za matibabu ya ndugu yetu Andrew Sanga ambayo imefunguliwa na rafiki wa Andrew anayejulikana kwa jina la Julius Shayo anayeishi Morrisville, North Carolina. Akaunti hiyo ina kichwa cha habari "Drew this Is How Much We Love You" https://dm2.gofund.me/pdzvn2hw. Familia ya Andrew haina uhusiano wowote na akaunti hii . Familia inaamini itakapofika muda wa kuhitaji msaada kwa ajili ya Andrew itafuata njia sahihi za kuwasiliana na jumuiya na marafiki wote wa mgonjwa.

Mchango wowote utakaotolewa kwenye akaunti hii uwe ni kwa mapendekezo binafsi ya mtoaji.

Ahsanteni sana

Cassius Pambamaji
Msemaji THC

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.