UPDATE - TAARIFA YA AJALI YA KAKA ANDREW SANGA


Hali ya ndugu yetu Andrew Sanga (Drew) aliyepata ajali jana bado siyo nzuri na yupo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Kwa mujibu wa msemaji wa familia Bw. Prosper Kiswaga madaktari wanategemea kumfanyia uchunguzi mwingine asubuhi hii ya leo kabla ya kutoa taarifa ya nini watakachokifanya kuhusiana na hali ya mgonjwa. Mgonjwa bado yuko katika hospitali ya Memorial Hermann Southwest, 7600 Beechnut St, Houston, TX 77074
Kwa mujibu wa Bw. Kiswaga, madaktari wanashauri kusiwe na mkusanyiko mkubwa wa watu hospitalini hapo hadi hali ya ndugu yetu Andrew itakapotengamaa.Taarifa zaidi zitawajia kila zitakapopatikanaAhsanteniCassius Pambamaji
Msemaji wa THC

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment