UPDATE YA MSIBA WA ANDREW SANGA HUKO MAREKANI.

Ndugu Wanajumuia na marafiki,

Kufuatilia msiba wa ndugu yetu Andrew Sanga hapo jana tarehe 20/04/2016, Wanajumuia chini ta Rais David Mayocha,tulifanya mkutano wa dharura na kuunda kamati Maalumu ya Msiba na kamati zake ndogo kushughulikia na kuratibu taratibu zote kuhusiana na msiba huu mzito!

Pamoja na kushindwa kutengeneza bajeti inayoakisi mahitaji yetu, tunafahamu tunahitaji kukusanya michango ya pesa n.k kukamilisha zoezi hili.

Kamati ndogo ya Fedha chini ya Bw. Prosper Kiswaga imefungua akaunti mbili za benki pamoja na akaunti ya kielektronikali ya PayPal ili kuwezesha na kurahisisha ukusanyaji michango.

Kamati ya Fedha inategemea kuwa na bajeti halisi jioni ya leo kufuatia mkutano wa Wanajumuia wote nyumbani na Bw. Kiswaga kama tulivyotangaziwa na uongozi wa Jumuia.

Tutazidi kupashana habari kwa ukaribu zaidi kadri Kamati zifanyavyo maamuzi.

Hapa chini ni akaunti za benki maalumu kwa shughuli hii.

1) Wells Fargo,NA

Jina: Andrew's Fund Raiding
Akaunti namba: 1835489301

Namba ya ruti: 580800393

2) Bank of America (BoA)

Jina: Andrew's Fund Raising
Akaunti namba: 488052463903

Namba ya ruti: 111000025

3) Akaunti ya PayPal

ltibaigana@gmail.com (Lambert Tibaigana)

***HUKU TUKIOMBOLEZA, TAFADHALI TUKUMBUKE KUWA, ANDREW ALIISHI MAISHA YA FURAHA NA HURU BILA KUJUTIA!!! BASI NA TUMUENZI KWA KUWA NA FURAHA NA KUKUMBUKA NYAKATI TULIZOFURAHI NAYE PAMOJA!!!! NAAMINI ANATUCHEKA KWA KUHUZUNIKA

Kwa niaba ya Prosper Kiswaga, Mwenyekiti Kamati ndogo ya Fedha

Saidi Nusura, Katibu Kamati Maalumu ya Msiba.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment