BMG INAWATAKIA MAADHIMISHO MEMA YA MEI MOSI 2016.

Wapenzi Wasomaji wa Binagi Media Group "BMG" inayoundwa na Binagi Blog, Binagi Online Tv na Binagi Online Radio, tunapenda kuwatakia Maadhimisho Mema ya Maadhimisho Mema ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yanayofanyika kila tarehe Moja Mwezi wa Tano (Mei Mosi) kote duniani.

Maadhimisho haya hufanyika ili kutathimini mchango, mafanikio na changamoto zinazowakabiri wafanyakati katika sekta mbalimbali ambapo wale waliotekeleza vyema majukumu yao, hupongezwa kwa kupewa zawadi ili kuongeza chachu ya utendaji kazi kwa wafanyakazi wengine huku changamoto zinazowakabiri wafanyakazi ikiwemo mishahara duni, zikielezwa bayana ili kutafutiwa ufumbuzi.

Kitaifa hapa nchini, Maadhimisho haya yanafanyika Mkoani Dodoma, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.
BMG 2016, Kikazi Zaidi.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment