MATUKIO MBALIMBALI MWEZI APRIL , LONDON, UINGEREZA

Profesa Issa Shivji akiwa na mwanahabari Freddy Macha,  na mwananchi wa Uingereza aliyefanya kazi Tanzania zamani.
Naibu Balozi,Uingereza, Msafiri Marwa (kushoto) na Said Surur, Katibu Mwenezi wa Task Force ya Watanzania Uingereza (Tzuk- TF),  nje ya Westminster Abbey, Jumatatu 26 April 2016. Hii baada ya sala ya kuuombea na kuubariki Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Sala hii alisema , Mheshimiwa Marwa, “ ni suala la kijadi linalofanywa kila mwaka na Uingereza kwa mataifa yaliyoko jumuiya ya Madola...”
Afisa Balozi, Amos Msanjila, (wa kwanza kulia)  na baadhi ya Watanzania waliohudhuria sala ya Westminster Abbey kuubariki muungano wetu. Bw Msanjila alisoma pia kipengele cha  Biblia katika sala hiyo inayofuata dhehebu la Wanglikana.
Profesa Issa Shivji akieleza na kutathmini historia ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vipengele vyake, ukumbi wa chuo kikuu cha SOAS, jijini London, Jumatano 20 April, 2016. Kushoto kwake ni Mtanzania Aikande Kwayu. Prof Shivji vile vile ni mwenyekiti wa KAVAZI inayosimamia kumbukumbu za Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, alialikwa kuzungumza na Jumuiya ya Waingereza na Watanzania - British Tanza nia Society. BTs.
Westminster Abbey - ambapo wamezikwa wananchi, wafalme  na viongozi  muhimu na mashuhuri wa Uingereza.
SOAS -School of Oriental and African Studies- chuo cha lugha London.
Mtanzania mkazi Uingereza, Enos Bukuku,  akimuuliza swali, Profesa Shivji.
Mtanzania Aikande Kwayu akizungumza na mmoja wa washiriki wa mhadhara uliohutubiwa na Profesa Shivji.
Washairi wa “Bards Without Borders” toka mataifa mbalimbali walifanyiwa mahojiano na TV ya sanaa ya  Ufaransa , Arte. Mwaka 2016, sherehe za kutimiza miaka 400 ya maisha ya mwanafasihi na gwiji wa lugha ya Kiingereza , William Shakespeare.  Toka kulia:  Laila Sumpton (Uingereza) mpiga picha wa Arte TV, Barabara Lopez (Colombia)  na Freddy Macha.

Mshoni, mchoraji na mbunifu mavazi, Mtanzania mkazi Uingereza, Jasmine Kissamo akionesha moja ya kazi za magauni yake. Jasmine anatazamiwa kufanya onesho kitongoji cha Greenwich , kusini ya London mwezi Julai.
Watanzania walikuwa miongoni mwa washindi wa tuzo la kudumisha utamaduni na maisha ya Mwafrika Ughaibuni.  Hamida Mbaga ( wa tatu kulia) anayeendesha biashara ya mavazi, Manchester na Freddy Macha – tuzo la kuendeleza muziki na utamaduni. Kati kati ni mchoraji na mbunifu mavazi Jasmine Kissamo.
Moja ya bendi maarufu za vijana “Sunburst”- iliyovuma miaka ya Sabini- imekumbukwa miaka 40 baadaye baada ya Kampuni ya muziki Uingereza -Strut Records- kutoa albam zake tatu. Unreleased Radio Sessions (1973), TFC &Moto Moto 45’s (1973-76) na Ave Africa LP (1976). Kati ya vibao vikali vya Sunburst ni “Banchikicha”, “Ukuti Ukuti”, “Simba Anguruma”, “Enzi za Utumwani”, “Black is Beautiful”, Matatizo Nyumbani”, na “Kipato Sina”...zilizotungwa na kuimbwa na marehem Kassim Magati na James Mpungo. Kati wana Sunburst walioko bado hai ni mpiga besi- Bashir Idi Farhan (anayeishi na kupiga muziki Uarabuni).

Mmoja wa watafiti wa kazi hii ya kihistoria, Mholanzi Jumanne Thomas alinieleza albam hizi zitakuwa rasmi madukani Afrika Mashariki , masoko ya kimataifa na mitandaoni, 24 Juni, 2016.Picha na habari za Freddy  Macha

Share on Google Plus

About Gadiola Emanuel

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment