MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA AONGOZA KAMPENI YA USAFI JIJI LA DAR LEO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Naseeb Abdul "Diamond Platnumz " Simba , Ruge Mutahaba wa Clouds Fm na wengine wengi wakishiriki Kampeni ya Usafi Leo Dar ya Makonda 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiongoza maelfu ya Wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika matembezi maalum ya kampeni ya kuhamashisha usafi katika jiji hili #Dar es salaam Ya Makonda, Usijifanye Mstaarabu kuwa Mstaarabu. Karume, Ilala na kuishia katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema hataki kuwaona nyumbani kwake wasanii ambao wamekacha kuhudhuria kampeni yake ya usafi ambayo imezinduliwa Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam. Akizungumza katika uzinduzi huo, Paul Makonda ameonesha kusikitishwa na idadi ndogo ya wasanii waliojitokeza kuunga mkogo kampeni hiyo.

“Lakini nashukuru wasanii wote ambao wamejumuika nasi, na kwa kweli hiki ni kipimo cha kuwatambua marafiki zangu wa kweli ni wapi. Na mimi niwaambie tu, sitaki kuona msanii yoyote nyumbani kwangu ambaye hawezi kuniunga mkono kwenye mambo yangu ya maendeleo,” alisema Makonda.

“Sitaki hiyo tabia, nimemuona Steve Nyerere hapa amekuja akiwa amechelewa hilo ni onyo, ukirudia tena nakushughulikia. Huwezi kuwa rafiki yangu alafu kwenye mambo kama haya huhangaiki, wengine wanataka waombwe, eti mbona hujanipigia simu kuniomba nipost, we nani?. Swala la usafi siyo la serikali ni swala la kila mtu,” aliongeza Makonda.
Wasanii ambao walihudhuria uzinduzi huo ni, Mchizi Mox, Yamoto Band, Diamond na team ya Wasafi, Mwasiti, Queen Darleen, Salam TMK pamoja na Steve Nyerere wa bongo movies.
Katika hatua nyingine Makonda amevitaka vyombo vya usafiri jijini Dar es salaam kuwa na vifaa vya kuwekea uchafu.
Pia wamewataka wafanyabiashara siku ya Jumamosi, kufungua maduka yao saa 3 asubuhi ili muda wa asubuhi wautumie kwa ajili ya kufanya usafi.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.