MSANII SNURA AFUNGIWA KUJIHUSISHA NA SANAA, TCRA WAAGIZWA KUIFUTA VIDEO YA CHURA MTANDAONI

Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kuufungia wimbo na video ya Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Snura Mushi unafahamika kwa jina la CHURA kutokana na kutokuwa na maadili ya Mtanzania.

Wimbo huo pia umezuiwa kutumbuizwa mahala popote na kufungiwa kuchezwa kwenye redio na runinga nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya watu kutousambaza wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp na Istagram na kuongeza kuwa wale watakaokiuka agizo hilo watashtakiwa kwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao.

Pia Wizara hiyo, imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya Msanii huyo, mpaka pale atakapo kamilisha taratibu za usajili wa kazi zake zote kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Serikali imewataka wanasii mbali mbali nchini, kujiuliza mara mbili kabla ya kubuni kazi zao za sanaa.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment