MWANDISHI WA GLOBAL MAKONGORO OGING' AFARIKI, KUZIKWA RORYA.

makongoro
Makongoro Oging' enzi za uhai wake.
Makongoro (2)
Makongoro Oging’ enzi za uhai wake akimkabidhi msaada wa fedha Kundi Luhende (kushoto) katika Hospitali kuu ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar.
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, watayarishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, wamepata pigo kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging' aliyefariki jana jioni (Jumamosi) Mei 21, 2016 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu alikuwa akiendelea kwa matibabu akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam ambapo mauti yalimfika. Makongoro (1)
Makongoro Oging' enzi za uhai wake akiwa na wakili Mabere Nyaucho Marando (kushoto).
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana kusubiri taratibu za mazishi na msiba upo nyumbani kwake Tabata- Magengeni jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda kijijini kwao Wilaya ya Rorya mkoani Mara kwa ajili ya maziko. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Mungu ailaze roho ya marehemu Makongoro mahali pema peponi-Amina. Makongoro (3)
Makongoro Oging’ akiongea na baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Ualimu Chang' ombe, jijini Dar es Salaam walikuwa katika mgomo.

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment