PAPA WEMBA AZIKWA MJINI KINSHASA

Mamia kwa maelfu ya mashabiki walijitokezasiku ya jana Jumatano kumzika mwanamuziki mkongwe wa DRC, Papa Wemba.
Wemba, aliyezaliwa kwa jina la Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba huko Lubefu enzi za utawala wa Wabelgiji, alianguka na kupoteza maisha wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani kwenye tamasha nchinni Ivory Coast, April 24. Alikuwa na miaka 67.

Mwili wake uliagwa kwa siku tatu kwenye jengo la bunge la nchini hiyo mjini Kinshasa.
Makumi kwa maelfu pia walikusanyika mtaani mbele ya kanisa la Notre Dame du Congo Cathedral ambako misa ya mazishi ilifanyika. “Papa Wemba siku zote amekuwa idol wangu,” alisema JB Mpiana, kiongozi wa kundi la Wenge Musica.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment