SAKATA LA WAFANYAKAZI HEWA RC PAUL MAKONDA AMSIMAMISHA KAZI AFISA UTUMISHI ILALA

Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda amemsimamisha kazi Afisa Utumishi wa Manispaa ya Ilala kwa kutowagundua watumishi hewa 11.
Hadi leo katika Mkoa wa Dar wamefikia watumishi hewa 248 wamebainika Dar, waleta hasara ya Shilingi bilioni 3.7.
Tarehe 2 Mei Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda aliwapa kiapo cha kazi wakuu wa Idara zote za jiji la Dar pamoja na maafisa Utumishi wa halmashauri za jiji wasaini kiapo cha kazi mbele ya Mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya baada ya kubainika kutoa taarifa zisizo za kweli dhidi ya kuwepo kwa watumishi hewa katika idara zao baada ya kubainika watumishi hewa wengine 209 katika Uchunguzi wa Siku chache zilizopita.
Miongoni mwa masharti yaliokuwapo katika kiapo hicho ni kwamba iwapo ikigundulika kuwapo kwa watumishi hewa katika idara husika baada wiki moja, Afisa utumishi au mkuu wa idara hiyo atalipa gharama za mishahara iliyopotea, kushitakiwa kwa uhujumu uchumi, kuachishwa kazi lakini pia kufikishwa mahakamani.
Hatua ya kusaini na kula kiapo inatokana na baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa Utumishi katika jiji la DSM kudaiwa kutoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa mkoa Paul Makonda na wakuu wa wilaya za jiji hilo baada ya kutoa idadi ndogo ya watumishi hewa kwa mkoa wa dsm ambao walikuwa 74 tu, huku uhakiki wa sasa uliofanywa na tume maalum ukibaini watumishi hewa 209 ambao wametafuna kiasi cha takribani shilingi bilion 2.7
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment