SUMAYE ATEULIWA MJUMBE KAMATI KUU CHADEMA

Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu, ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA – Taifa amekiambia Kikao cha Kamati Kuu kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho.

Amesema, dhamira ya CHADEMA ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila mwanachama kufanya kazi ya uenezi.

Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Naye Fredric Sumaye amemshukuru Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa kumteua kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.

Source: Swahili Times
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment