COCA-COLA KUENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA UMISSETA NCHINI TANZANIA

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akikagua wachezaji wakati wa Uzinduzi wa mashindano ya UMISETA ambayo mwaka huu yamedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola. Uzinduzi huo ulifanyika May 10, 2016 katika uwanja wa Sokoine ambapo kulifanyika michezo na burudani mbali mbali. --- Mashindano kwa ajili ya fainali za kitaifa za Copa-UMISSETA ambayo yanadhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, na ambayo yalipangwa kuanza kufanyika siku ya leo hadi hapo tarehe 24 Juni 2016 yametangazwa kuahirishwa. Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa hapo jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), George Simbachawene, serikali imechukua uamuzi huo ili kupisha utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la upatikanaji wa madawati, ambao kikomo chake ni mwisho wa mwezi huu. Mashindano haya ya fainali za Copa-UMISSETA yalilenga kuzikutanisha timu za mikoa mbalimbali nchini kwa pamoja Jijini Mwanza, zikiwa zimeundwa na wachezaji mbalimbali kutoka shule za sekondari ili wachuane kwenye michezo na sanaa.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke - Dar es Salaam, Sophia Mjema (kushoto), akisalimiana na wachezaji wa timu ya Makongo Sekondari katika Mashindano ya UMISETA ambapo kampuni ya Coca Cola ndiyo walikuwa ni wadhamini wakubwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016. --- “Thamira yetu katika kudhamini mashindano haya na kushirikiana TAMISEMI iko pale pale, tukiwa tumejidhatiti kuendelea kuunga mkono jitihada za kutambua na kuinua vipaji vya vijana ambao watakuja kuifikisha Nyanja ya michezo nchini katika kiwango cha juu zaidi. Tutaendelea kuunga mkono na kusaidia kukua kwa sekta ya michezo nchini, hususani mashindano ya mpira wa miguu pamoja na mpira wa kikapu kwa vijana,” alisema David Karamagi, Mwakilishi Mkazi wa Coca-Cola Tanzania. Karamagi aliongeza kuwa kampuni ya Coca-Cola Tanzania inayo imani ya dhati na ikiamini ya kwamba mashindano ya michezo yanayoanzia ngazi ya chini kabisa ndiyo namna thabiti nay a kipekee katika kuibua vipaji vya wachezaji nchini. Pia Karamagi alisema kuwa, wakati wadau wakisubiri kwa hamu kutangazwa kwa tarehe mpya za kurejewa kwa fainali za mashindano haya nchini, Coca-Cola Tanzania ilishajipanga kudhihirisha ya kwamba michezo ni zaidi ya ushindani, kwa kuweza kuambatanisha mashindano haya na kujenga mshikamano wa timu shindani, urafiki na hata nidhamu kwa wachezaji na timu za mikoa inayoshiriki. Hivyo basi, kwa udhamini ulioingiwa mwaka huu, Coca-Cola Tanzania itaweza kupanua wigo wa ushirikishwaji wa michezo murua zaidi mbali ya mpira wa miguu, hasa kwa kuweza kujumuisha mpira wa kikapu. “Kampuni ya Coca-Cola nchini tutaendelea na dhamira yetu ya kuunga mkono jitihada ya vijana mbalimbali nchini kote katika kuwasaidia kudhihirisha vipaji vyao kupitia mashindano mbali mbali ya michezo, ikiwa ni pamoja na UMISSETA na Copa Coca-Cola’” alimalizia Karamagi.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment