Dk Shein Awaapisha Manaibu Katibu Wakuu Ikulu Zanzibar leo.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
 Zanzibar                                                                  28.6.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewapisha viongozi mbali mbali kushika nyadhifa katika taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Walioapishwa ni Dk. Islam Seif Salim kuwa Naibu Katibu Mkuu, Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ambapo kabla ya wadhifa huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu iliyokuwa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Hassan Abdulla Mitawi ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Habari katika Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo ambapo kabla ya wadhifa huo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Zanzibar (ZBC). 

Aidha, Dk. Shein amemuapisha Rafii Haji Makame kuwa Katibu Mtendaji Tume ya  Utangazaji Zanzibar katika Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo ambapo kabla ya wadhifa huo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo katika Wizara hiyo.

Hafla ya kuwaapisha viongozi hao ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu, Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma. 

Viongozi wengine ni na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid, Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Chumu Kombo Khamis, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum.

Wengine ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali. 

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822  
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment