MSASA WA SDGS WAENDELEA UDOM, VITIVO VYAKAMILIKA

Mtaalamu wa mawasiliano katika Ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiendesha mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani (SDGs) kwa nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma kwa wanafunzi wa vitivo mbalimbali na walimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyomalizika jana chuoni hapo.(Picha na Modewjiblog)

Ninajisikia kuelimika na kuelewa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu kiasi ya kwamba ninaweza sasa kuwaelimisha marafiki, vijana wenzangu na familia. Elimu hii hapo awali sikuwa nayo, sikuwa naelewa vyema malengo haya. Ukomo wa mpango huu wa dunia ni mwaka 2030 wakati ambapo mimi nitakuwa na umri wa miaka 40. Nataka kuwa sehemu ya mashuhuda wa mafanikio katika utekelezaji wake na ndio maana nataka kutimiza wajibu wangu kwa kupeleka elimu hii kwa wengine.” anasema Jane, mmoja wa washiriki wa semina.

VIJANA 1000 na wanazuoni 200 wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) wamepatiwa mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani kwa nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma.
Kazi ya kufunza malengo hayo ilifanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi ya Umoja wa Mataifa (UN) kuwezesha uelewa kwa tumaini kuwafanya wananchi hasa vijana kutambua wajibu wao katika kutekeleza malengo hayo.
Mafunzo hayo katika Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ni mwendelezo wa mafunzo yaliyozinduliwa Arusha wiki iliyopita na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez.

Mafunzo hayo yalifanywa kwa kundi la vijana 50 kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania ili waende kusambaza uelewa wa malengo hayo kwa vijana wenzao nchini kote.

Inatarajiwa kuwa zaidi ya vijana elfu 20 watakuwa wamepatiwa mafunzo katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.

Akizungumza katika kampasi ya UDOM Bw. Rodriguez alisema kwamba Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanahitaji ushirikiano wa watu wote ili kuyafanikisha kama ilivyokusudiwa. Malengo ya Maendeleo Endelevu ukomo wake ni mwaka 2030.

Aliwapongeza wanachuo na wanazuoni kwa kujikita kwao kuelewa Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo ndiyo malengo ya dunia ili kuweza kuyasimamia na kuyatekeleza.

Pia alizungumzia umuhimu wa vijana kushiriki katika masuala ya maendeleo hasa kwa kuzingatia kwamba asilimia 60 ya wananchi wa Tanzania ni vijana.

“Mna wajibu mkubwa kwa vijana wenzenu” alisema Bw. Rodriguez na kueleza kwamba amefurahishwa kuona kwamba vijana na wanazuoni 1,200 wameahidi kuwa walimu na mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu majumbani kwao, katika taasisi zao na katika jamii inayowazunguka.
Pichani juu na chini ni Sehemu ya wanafunzi na walimu wa UDOM wakimsikiliza mkufunzi Hoyce Temu (hayupo pichani) kwa makini wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyomalizika jana chuoni hapo.

Alisema katika hilo Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kuhakikisha kwamba wake kwa waume na vijana wanatekeleza wajibu wao kwa kushiriki vyema katika mipango ya maendeleo yenye kulenga kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu duniani.
Alisema wajibu wa kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu duniani kunategemea watu wote na hasa vijana.

Akipongeza juhudi za kuelimisha za Umoja wa Mataifa, Profesa Flora Fabian kutoka UDOM, alisema chuo hicho kimefurahishwa kuwa moja ya vituo vya kufunza mabalozi vijana wa kusambaza elimu na wajibu katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Alisema malengo hayo ya Dunia ni lazima yajulikane kwa kila mmoja; huku akiwataka wanazuoni kuyazungumza katika kazi zao za kila siku, katika tafiti na ripoti kama ilivyo kwa wanafunzi ambao wanastahili kupikwa kuwa katika nafasi ya kuweza kuchambua malengo hayo kwa kuwa na takwimu na taarifa sahihi.

Alipongeza uamuzi wa utoaji elimu wa Umoja wa Mataifa na kuamini kwamba watasambaza elimu hiyo kwa vyuo vikuu vyote nchini Tanzania.

Septemba 2015, viongozi kutoka nchi 193 duniani walitia saini Malengo ya Maendeleo Endelevu duniani. Malengo hayo mapya yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15 huku ikiweka pamoja shughuli za maendeleo ya kijamii, kiuchumi yanayojali mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Mmoja wa wanafunzi wa UDOM akipitia makabrasha ya SDGs wakati wa mafunzo hayo.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Muya Said akitoa maoni wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini na kumalizika jana chuoni hapo.
Mwanafunzi wa Digrii ya kwanza ya Mifumo ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Janeth Dutu akiuliza swali kwa mkufunzi wa mafunzo hayo (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini na kumalizika jana chuoni hapo.
Mkufunzi wa mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs), Hoyce Temu akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo wakati zoezi la maswali na majibu.
Mhadhiri Msaidizi wa Maendelelo ya Jamii katika Chuo cha Sayansi za Jamii, Sanaa na Lugha (CHSS) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Angelo Shimbi akitoa maoni wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini na kumalizika jana chuoni hapo.
Beatrice Mkiramweni kutoka Ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, akipitia makabrasha ya SDGs wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini na kumalizika jana chuoni hapo.
Mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yakiendelea chuoni hapo.
Kutoka kushoto ni Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Development Studies -UDOM, Edson Baradyana, Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa, Mtaalamu wa Upangaji na Usimamizi wa Miradi -PRO UDOM, Radhia Rajabu, Mhitimu wa kidato cha sita, Aisha Msantu wa Asasi ya Vijana wa Umoja Taifa Tanzania (YUNA) katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Kutoka kushoto ni Mtaalamu wa mawasiliano katika Ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu, Mhitimu wa kidato cha sita, Aisha Msantu wa Asasi ya Vijana wa Umoja Taifa Tanzania (YUNA) pamoja na Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa katika picha ya ukumbusho mara baada ya kuhitimisha mafunzo.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi wa UDOM walioshiriki kwenye mafunzo ya SDGs yaliyomalizika jana chuoni hapo. (Picha zaidi ingia hapa)
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment