TAHLISO WAMSHUKIA GWAJIMA

SHIRIKISHO LA WANAFUZI VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA LALAANI KAULI ZA GWAJIMA JUU YA VIONGOZI WA CCM
Katibu wa TAHLISO Siraji Madebe akizungumza leo
DAR ES SALAAM
Siku chache baada ya Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kuwashutumu viongozi wa CCM kwamba wanamipango ya kutomkadhi chama Rais Dk. John Magufuli, Shirikiho la Wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), limemshukia na kulaani vikali kauli hiyo kwamba ni yauchochezi.


Akizungumza leo latika Ofisi za Shirikisho hilo, jijini Dar es Salaam, Katibu wa TAHLISO Siraji Madebe, amesema, Gwajima kama kiongozi wa dini ajitokeze hadharani kutaja viongozi anaodai walimpigia simu kuelezea mkakati huo wa kutomkabidhi Chama Dk. Magufuli.


SOMA TAARIFA KAMILI KAMA ILIYOTOLEWA NA TAHLISO
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania limeshitushwa na taarifa za uchochezi zilizotolewa na kiongozi wa dini wa kanisa la Ufufuo na Uzima hivi karibuni likituhumu viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuwa na mipango ya kutokumkabidhi Chama Raisi  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh. John Joseph Pombe Magufuli.


Sisi kama Vyuo Vikuu tunalaani vikali sana kauli yenye dalili za uchochezi zinazotaka kupandikiza chuki miongoni mwa viongozi wetu wa Serikali  na Chama kwa ujumla.Lakini kama kiongozi wa dini mwenye hofu ya Mungu tunamtaka ajitokeze kuwataja hadharani wale waliompigia simu kumuomba awasaidie bila kuwasahau na wale wanaozunguka mikoani kwa ajili ya kuhamasisha zoezi hilo kama alivyoeleza.Ndugu waandishi wa habari, pamoja na mambo mengine kwa faida ya watanzania kiongozi huyu angetaka ufafanuzi juu ya jambo hili angewasiliana na katibu wetu wa Chama cha Mapinduzi Comrade Abdulrahman Kinana au Naibu Katibu Mkuu wetu wa Chama Cha Mapinduzi Comrade Rajab Luhavi badala ya kwenda kuaminisha waumini na watanzania jambo lisilokuwa na uhakika.Lakini ndugu zangu katika maelezo yake alidhihirisha wazi kwamba hakiungi mkono Chama Cha Mapinduzi na pia hakumuunga mkono mhe. Rais katika kipindi cha kampeni, hivyo asichukue nafasi hiyo ya kutaka kugombanisha na kukisambaratisha Chama Chetu.Tunatoa rai kwa viongozi na Taasisi za kidini zote nchini kutojihusisha na masuala ya kisiasa na badala yake kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa kwa uwepo wao. Kuhusisha siasa na dini ni kuchochea uhasama na kupandikiza mbegu za chuki, vurugu, uchochezi na kuhatarisha uvunjifu wa amani baina ya wananchi, viongozi na Taifa kwa ujumla. Hivyo hatuko tayari kuwavumilia watu wote wenye nia ya kutuvurugia amani tuliyo nayo na kutuingiza kwenye migongano ya kidini.Tanzania ni moja na watanzania ni wamoja bila kujali tofauti za kisiasa, kidini na kikabila.Mwisho tunapenda kuiomba serikali kupitia vyombo vya dola kushughulikia kwa kina jambo hili na kulichukulia hatua ili kukomesha vitendo vya uchochezi baina ya watanzania na baina ya viongozi.

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment