BARAZA LA WAZEE WA CHADEMA LAMUOMBEA RAIS MAGUFULI AFYA NJEMA.

Rais Magufuli akigawa sambusa kwa maafisa waandamzi wa polisi baada ya hafla ya kula kiapo cha uadilifu Ikulu Dar. Picha ya Issa Michuzi
BARAZA la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limemuombea dua Rais John Magufuli awe na afya njema na aendelee kutumikia katika misingi inayompendeza Mungu.

Dua hiyo ilitolewa jana ikiongozwa na Mwenyekiti wa baraza hilo, Hashim Juma katika mkutano na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kueleza namna ambavyo hawaridhishwi na mwenendo wa utendaji kazi wa Rais Magufuli na yaliyojiri Zanzibar.

Hashim alisema pamoja na kwamba baraza hilo haliridhishwi na mwenendo wa Rais Magufuli, limeamua kumuombea dua kwa sababu rais mwenyewe aliomba kuombewa. “Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ampe afya njema, ampe maisha marefu na amjalie aongoze katika misingi anayopenda yeye, amina,” alisema Hashimu wakati akiongoza dua na wazee wengine kuitikia amina.

Hata hivyo, awali Hashim aliituhumu serikali ya Magufuli akisema inakandamiza upinzani na pia haendeshwi katika misingi ya kidemokrasia. “Katika mkesha wa Krismasi mwaka jana, Rais aliomba tumuombee dua, kwa sababu ameomba mwenyewe na jambo hili la kuomba dua ni jambo kubwa, hatuna budi kumuombea,” alisema Hashim.

Alisema Rais Magufuli amekuwa na kauli tata ambazo amekuwa akizungumza hadharani lakini viongozi na wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kukemea na wao hawawezi kukaa kimya.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment