MWIGULU NCHEMBA ASHIRIKI KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI, AWATAKA WASHIRIKIANE NA SERIKALI KUPAMBANA NA UHALIFU NCHINI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu (BAKWATA), Suleman Said Lolila wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Viongozi wa Dini lililojadili masuala ya ugaidi. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na viongozi wa dini kuhusu masuala mbalimbali ya amani nchini katika Kongamano la Viongozi wa Dini lililofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake, Waziri Mwigulu aliwataka viongozi hao kutokuhusisha kosa lifanyalo na mtu au watu fulani kulifananisha na dini yake, amewaomba viongozi hao watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa za matukio mbalimbali ya kiuhalifu nchini. Kutoka kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Paul Ruzoka, Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeiry Bin Ally na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Leonard Mtaita. 
Sehemu ya viongozi wa dini walihudhuria katika Kongamano la Viongozi wa Dini nchini lililofanyika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment