BASATA WAMFUNGULIA NEY WA MITEGO.

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limemfungulia Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego kuendelea na shughuli za Sanaa baada ya kuwa ametekeleza adhabu (maagizo) zote alizopewa kama masharti ya kumfungulia.

Vilevile Basata kama mlezi wa wasanii linamfungulia kufuatia yeye mwenyewe (Nay wa Mitego) kujutia na kukiri kwamba amejifunza na yuko tayari kubadilika na kwamba hatarudia makosa aliyoyafanya.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngeneza umeeleza kuwa pamoja na kumfungulia kuendelea na shughuli za Sanaa Baraza linamweka kwenye uangalizi maalum msanii huyo kama sehemu ya kuhakikisha anaendesha shughuli za Sanaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu sambamba na kuzingatia maadili katika kazi zake.

Source: Mwananchi
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.