MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE WA TAASISI YA HANS SEIDEL JIJINI DAR ES SALAAM

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya HANNS SEIDEL kutoka nchini Ujerumani Profesa Ursula Mannle (kushoto)ambaye ameongoza ujumbe wa watu wanne akiwemo Waziri wa Nchi, Kazi, Masuala ya Kijamii wa Bavaria   Mhe. Emilia Muller walipometembelea Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Shirikaka la HANNS SEIDEL kutoka nchini Ujerumani Profesa Ursula Mannle (kushoto) pamoja na Waziri wa Nchi, Kazi, Masuala ya Kijamii wa Bavaria   Mhe. Emilia Muller walipometembelea Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu (katikati) Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka Taasisi ya HANNS SEIDEL la Ujerumani,Wengine pichani ni Waziri wa Nchi, Kazi, Masuala ya Kijamii wa Bavaria   Mhe. Emilia Muller ( kulia)  Mwenyekiti wa Taasisi ya HANNS SEIDEL kutoka nchini Ujerumani Profesa Ursula Mannle (kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Taasisi HANNS SEIDEL Bi. Julia Berger( wa pili kushoto),Meneja wa Mradi Kadele Mabumba (wa pili kulia),
Ikulu jijini Dar es Salaam


                                            .................................................................. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameitaka Taasisi ya Hans Seidel Foundation isaidie kupeleka Elimu ya Uraia bungeni ili wabunge wajue wajibu wao ndani na nje ya Bunge.

Mhe. Samia ametoa kauli hiyo leo baada ya kukutana na ujumbe wa Taasisi ya Hans Seidel Foundation uliomtembelea ofisi kwake Ikulu, Jijini Dar es salaam kutaka kujua kama ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna sheria na kanuni za kuendesha vikao vya Bunge. 


Makamu wa Rais aliueleza ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Hans Seidel Foundation Prof. Ursula Mannle kuwa sheria na kanuni zipo za kuendesha vikao vya Bunge lakini baadhi ya wabunge hawazifuati kama inavyotakiwa.

Alisema kwa mtazamo wake elimu ya uraia itasaidia katika kuwafanya wabunge hao wajenge nidhamu katika michango na ushiriki wao kwa ujumla ndani na nje ya Bunge.

Akizungumzia kuhusu kuanzishwa kwa dawati la jinsia katika vituo vya polisi Mheshimiwa Samia alisema ni hatua nzuri kwani wanawake kwa sasa wako huru kueleza wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia tofauti na ilivyokuwa hapo awali. 


"Kwa sasa wanawake wanakutana na wanawake wenzao wako huru kuzungumza wanaporipoti matukio ya kupigwa na haki inatendeka bila ya hata kutoa rushwa. Kuna mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi kwa upande huo," alisema Mhe. Samia.

Alisema kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha watu wote wanaoenda kinyume na taratibu wanachukuliwa hatua za kisheria na kusema kwenye utumishi wa umma mambo yamebadilika kiasi kwamba makusanyo ya kodi yameongezeka Serikalini.Taasisi ya Hans Seidel Foundation yenye makao yake makuu Munich, nchini Ujerumani ambayo inajishughulisha na masuala ya demokrasia, amani na maendeleo huku ikitoa kipaumbele kwenye elimu ya uraia inaendesha shughuli zake katika nchi zaidi ya 60 duniani.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment