MCHUNGAJI DKT.DANIEL KULOLA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA MWANZA KUITETEMESHA INJILI KWA MARA NYINGINE NCHINI MAREKANI.

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Jijini Mwanza, akihubiri katika moja ya mikutano yake iliyofanyika mkoani Morogoro.

Kwa mara nyingine Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola, amepata kibali cha kupeleka neno la Mungu katika bara la Amerika.

Itakumbukwa kwamba ni miezi michache tu baada ya kupata kibali kama hicho ambapo alihubiri katika majimbo ya Dallas, Houston, Fortworth, Boston, Connectcut, Ohio Cincinnati na New York nchini Marekani.

Pia Dkt.Kulola, alipata kibali cha kuhudumu nchini Canada katika Kanisa kubwa la The Global Kingdom pamoja na miji mbalimbali kama vile Ottawa, Quebec na Toronto.

"Watu wengi walibarikiwa na kuinuliwa kimwili na kiroho kwani injili yangu ni kuyashughulikia maisha ya watu kiroho na kimwili". Anasema Dkt.Kulola ambaye awamu hii amepata kibali cha kuhudumu katika miji ya Boston, Dallas na Arizona nchini Marekani.

"Nataraji Bwana atatenda mambo makubwa huko, ninaomba maombi yenu kwa nguvu zote". Anadokeza Dkt.Kulola na kuwasihili watakaohitaji kuwasiliana nae watumie nambari za simu +255 767 749 040 kwa Tanzania na +1 832 777 5032 kwa Marekani.

Huduma za Mchungaji Dkt.Kulola zinatarajia kuanza agost 09,2016 nchini Marekani na kufikia tamati Agost 25,2016 ambapo safari ya kurejea Tanzania itakua imewadia.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Jijini Mwanza, akihubiri katika moja ya mikutano yake iliyofanyika barani Amerika.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment