MHANDISI MASAUNI AZINDUA MKAKATI WA BARAZA WA KUKABILIANA NA AJALI ZA BARABARANI NCHINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Baadhi ya mambo yaliyolengwa katika mkakati huo ni pamoja na udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwa uzembe, udhibiti wa mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa magari pamoja na kuanza utaratibu wa Mfumo Nukta (point system) kwenye leseni za udereva ambapo dereva akifanya makosa kadhaa atanyang’anywa leseni na kutokuruhusiwa kuendesha gari tena. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda Mohammed Mpinga. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda Mohammed Mpinga. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.