MTATURU: WANANCHI WANATAKIWA KUFUGA KUKU SIO KUISHI NA KUKU

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la maonesho ya Nanenane la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa Rehema F. Malila kutoka Kijiji cha Unyangwe, Kata ya Iseke ya namna usindikaji unavyofanyika Wilayani humo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akipata ufafanuzi kutoka kwa Mratibu wa Mfuko wa Afya ya jamii (CHF) Edward Bulilo Maselo alipotembelea banda la maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Singida juu ya umuhimu wa jamii kujiunga na mfuko huo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akipata maelekezo ya ufugaji wa kisasa wa kuku kutoka kwa mfugaji aliyefanikiwa katika ufugaji Madai Njou anayetokea Kijiji cha Nyangwe, Kata ya Iseke baada ya kupatiwa mafunzo kutoka Idara ya Kilimo na ufugaji ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua kuku waliofungwa kisasa ambapo jogoo mmoja aliyefikisha umri wa mwaka mmoja anauzwa shilingi 20,000
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akinunua Asali kwa ajili ya matumizi yake baada ya kuvutiwa na asali hiyo iliyopo kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Dc Mtaturu akikagua chakula cha kuku kinachotengenezwa na Uyanjo Vicoba Group ya Wilayani Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu (mwenye suti), Kulia kwake ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Hassan Tati, kushoto kwake ni Ally Mwanga ambaye ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilayaya Ikungi, Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya yaikungi, na Wajasiriamali kutoka katika Halmashauri ya Wilaya hiyo

Na Mathias Canal, Dodoma
Wananchi wametakiwa kujihusisha na ufugaji wa kuku kwa njia za kisasa ili waweze kujipatia kipato kupitia mayai ama kuuza kuku mwenyewe ili kuondokana na dhana ya kuishi na kuku ilihali wanajigamba kama wafugaji wazuri.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika maonesho ya Nane nane yanayofanyika katika Uwanja wa Nzuguni Kanda ya Kati Dodoma ambayo yanataraji kufikia kilele hapo kesho.
Mtaturu amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi Wilayani humo na Taifa kwa ujumla wanajihusisha na shughuli za Kilimo na ufugaji lakini aina ya ufugaji wanayoitumia ni ile iliyopitwa na wakati na kuishi na mifugo ndani badala ya kuijengea eneo la banda ambalo ni pana na maalumu kwa ajili ya ufugaji.
Dc Mtaturu amewataka wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika idara ya kilimo kutoa elimu kwa wananchi juu ya mazao makuu ya biashara yanayostahimili mvua ili kupata mazao ya kutosha na kuyauza kwa wakati tofauti na mazao mengine ambayo yanalimwa kila maeneo hivyo kupunguza gharama halisi ya bei.
Amewataka pia wataalamu hao kuhakikisha elimu wanayoitoa kwa wananchi inakuwa sambamba na kuwashauri wananchi kulima zao la mtama wa muda mfupi aina ya Hakina na Macia.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayoub Yusuph amesema kuwa ofisi yake itatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa Wilaya hiyo ili kuwainua zaidi wananchi ambao wanalima na kufuga lakini sio kilimo na ufugaji wa kisasa jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.
Yusuph alisema kuwa katika maonesho hayo wamewaalika wakulima na wafugaji ambao wamefanikiwa katika kilimo na ufugaji wao baada ya kupata mafunzo kutoka katika ofisi yake ili kushuhudia na kuelezea mbinu walizopatiwa na namna zilivyowasaidia.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment