NYUMBA ZOTE ZILIZOJENGWA KWENYE HIFADHI YA RELI NA BARABARA KUU ZOTE NCHINI KUANZA KUBOMOLEWA

Meneja wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Mkoa wa Mbeya Bw. Fuad Abdallah akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu uharibifu wa Daraja la Reli ya TAZARA eneo la Mbalizi Mkaoni Mbeya kutokana na shughuli za kibinadamu, alipotembelea daraja hilo leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi wa karakana ya Mbeya.

Serikali imeiagiza Mamlaka ya Reli ya Tanzani na Zambia (TAZARA), Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), zianze kubomoa nyumba zote zilizojengwa kwenye hifadhi  ya reli na barabara kuu zote nchini ili kuilinda miundombinu hiyo isiharibiwe.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa mkoani Mbeya mara baada ya kukagua  Daraja la Reli ya Tazara  lililopo Mbalizi nje kidogo ya mji huo na kusisitiza umuhimu wa wananchi kulinda miundombinu “Sheria iko wazi, lazima muisimamie msisubiri mpaka Waziri aseme. Mwananchi yeyote aliyeifata miundombinu ya reli lazima mmvunjie nyumba yake ili miundombinu iliyojengwa kwa kutumia fedha nyingi iweze kudumu”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema Serikali ipo katika hatua za kuboresha miundombinu ya reli ya kati na reli ya Tazara ili kuhakikisha mizigo yote ya ndani na nje ya nchi inayopitia kwenye bandari ya Dar es Salaam na kupita katika barabara inapita katika reli.

“Mizigo inayopita katika reli ni asilimia 4 tu kutoka bandarini hivyo lazima tujipange kuanza kutafuta masoko na kuchukua mizigo hiyo ili kulinda miundombinu ya barabara inayoharibiwa na uzito mkubwa”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha Waziri Prof. Mbarawa ameuhimiza uongozi wa TAZARA kuongeza juhudi katika utoaji elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya uchimbaji mchanga, kokoto kwenye hifadhi ya miundombinu ya reli hasa kwenye mito na chini ya madaraja ili kuzuia uharibifu kuhatarisha usalama wa usafiri wa treni.

Naye Meneja wa TAZARA wa mkoa wa Tanzania Bw. Fuad Abdallah amemueleza Waziri Mbarawa zoezi la kubomoa nyumba litatekelezwa kama  sheria ya reli inavyosema kwa wananchi kuacha  ya mita 30 kwa vijijini na mita 15 kwa mjini.

Ameongeza kuwa mamlaka itaendelea kutoa elimu ya utunzaji wa  miundombinu ili wawe sehemu ya utunzaji kwa kuacha kufanya shughuli zao kwenye maeneo hayo.

Katia ziara hiyo, Waziri Prof. Mbarawa amekagua pia  Karakana ya TAZARA ya Mbeya ambayo inatoa huduma ya matengenezo ya vichwa vya treni 39 aina ya Diesel Electric (DE) pekee na kubaini ukosefu wa baadhi ya mitambo, uchakavu wa mitambo iliyopo na ukosefu wa vipuri.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua mashine ya kichwa kimojawapo cha treni wakati alipokagua ukarabati wa vichwa hivyo katika karakana ya Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na mmoja wa abiria wakati alipokagua huduma za Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA), (hawapo pichani) wakati alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Mbeya.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), wakati alipozungumza nao, Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza maoni kutoka kwa wakazi wa Lyunga, Mbeya mara baada ya kumaliza kuongea na wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza maoni kutoka kwa wakazi wa Lyunga, Mbeya mara baada ya kumaliza kuongea na wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) Mkoani Mbeya.

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.