WAKINAMAMA WATAKIWA KUNYONYESHA KUEPUKA SARATANI YA TITI NA WATOTO KUWA NA AKILI.

Mama akiwa ananyonyesha mtoto. Picha ya mtandaoni
 
Na Woinde Shizza, Arusha  
Wakinamama wanaonyonyesha nchini wametakiwa kuwanyonyesha watoto wao kwa muda uliopangwa kitaalamu ili kuweza kuepuka kupata magonjwa na saratani ya titi,kuwa na msongo wa mawazo sambamba na ukuaji usiostahili hali ambayo mtoto anakuwa na uelewa mdogo hasa darasani ambapo hali hiyo isiposimamiwa na wazazi pindi wawanyonyeshaji itaathiri sana maisha ya mtoto huyo. 

Ambapo aliongeza kuwa hivi sasa wakinamama wengi hawawanyonyeshi watoto wao kipindi kilichopangwa kwa muda wa miaka miwili ambapo kutokana na hali ngumu ya maisha na kuwa watu wamnekuwa wakijishughulisha sana ili kuweza kutafuta riziki zao wamekuwa wakinyonyesha sichini ya miezi tisa tu hali hiyo ama madhara yake hayaonekana mapema hasa kipindi mtoto akianza shule nahasa katika matokeo yake ya kimasomo kushuka na hata kutoelewa kwa haraka kama watoto wengine wakawaida. 
 

Hayo yameelezwa leo katika mahojiano maalumu wakati wa tathmini ya hali ya unyonyeshaji na Afisa lishe wa wilaya ya Meru bi,Asia Ijumaa wakati akitoa somo kwa kinamama wakati wa clinik ya kinamama na watoto katika hospitali ya Patandi iliyoko tengeru wilayan Meru mkoani Arusha. 
 
Hata hivyo alisema kuwa mbali na jitihada zakutoa elimu kwa wakinamama hao lakini bado wanakabiliwa na changamoto kubwa sana ikiwemo kushuka kwa kwa hali ya unyonyeshaji ambapo kwa sasa ni asilimia 32 tu ambapo ukilinganisha na na unyonyeshaji kwa nchi zilizoendelea ambapo ni asilimia 39 hali ya unyonyeshaji sio nzuri ukilimnganisha na mahudhurio ya kinamama kupata elimu yao. 
 
Aidha bi Asia amewashauri wakinamama wote kuweza kuzingatia elimu ya kunyonyesha watoto ambapo mtoto kuanzia siku sifuri hadi miezi sita hatakiwi kupewa kitu chochote kila ambapo baada ya muda huo anatakiwa kuanza kupewa changanyiko wachakula na mlo kamili ili kuweza kumjenga katika nlishe na kiakili pia. 
 
Kwa upande wake mmoja wakinamama bi,Sofia Boma alisema kuwa kuna hjaja sasa watatalamu wa lishe waendelee kutoa elimu kwa kushirikiana na wizara ya afya ili kuweza kusaidia malezi na makuzi ya watoto hao katika kulinda maisha yao. 
 
Pia amewataka wataalamu walishe kuweza kuweka utaratibu wakuwafatilia wakinamama wanaonyesha ili kuwaangalia mienendo yao ili kuweza kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri katika kunyonyesha watoto wao.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.