WANADIASPORA 350 KUHUDHURIA KONGAMANO ZANZIBAR


By Haji Mtumwa, Mwananchi hmtumwa@mwananchi.co.tz

Zanzibar. Zaidi ya wanadiaspora 350 wanatarajia kuhudhuria kongamano lao mwishoni mwa mwezi huu lengo likiwa kuwaunganisha na Serikali kutafuta njia mbadala ya kuleta maendeleo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Salum Maulid Salum amesema jana kuwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kongamano hilo.

“Tunatarajia kuwa mada zitakazowasilishwa katika kongamano hili la siku mbili zitasaidia kutoa michango ya kuimarisha uchumi wa pande zote mbili kwa Serikali ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema.

Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Silima Kombo Haji amesema makongamano ya wanadiaspora yana faida nyingi kwa jamii na Taifa.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment