Makonda amtaka DC wa Temeke kutafuta njia ya kutatua uhaba wa madarasa 2568

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix J Lyaniva kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa 2568 ambayo yanahitajika katika wilaya hiyo baada ya kufanikiwa kutatua changamoto ya madawati.

 Akiongea Jumatatu hii ndani ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Temeke katika ziara yake ya siku kumi ya kusikiliza changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, Makonda amemtaka DC huyo kutafuta namna ya kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa kwa kutafuta wadau ambao watajenga madarasa hayo kwa utarabitibu wa kuwalipa taratibu.

RC Makonda ( kulia) akiwa na DC wa Temeke, Felix Lyaniva

“Mnatakiwa kutafuza njia ya kujenga haya madarasa kwa njia yoyote ili haya madawati yaliyotengenezwa yasiharibike,” alisema Makonda. “Kwahiyo nakuagiza mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi wako tafuteni wadau ambao mtashirikina nao katika ujenzi wa haya wa madarasa kwa ajili ya vijana wetu. Sio tu kukopa pesa benki pia mnaweza kutafuta wadau ambao wanaweza kujenga halafu mkawa mnawalipa taratibu,”
RC Makonda alitoa kauli hiyo baada ya DC wa Temeke kumtaarifu Mkuu huyo kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa madarasa 2268 ya shule ya msingi na 300 ya shule za sekondari.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment