Miss Africa 2016,Tanzania Itawakilishwa na Julitha Kabete Chini ya Millen Magese Group Ltd

Mashindano ya Miss Africa yatafanyika Nigeria na Tanzania itawakilishwa na Julitha Kabete .Alisema mengi kupita kwenye ukurasa wake wa instagram.


Naitwa Julitha Kabete. Ni mrembo ambaye nitawakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya kufatuta mrembo wa Afrika 2016. Mashindano haya yatafanyika nchini Nigeria, jimbo la Cross River state mjini Calabar tarehe 26, novemba 2016. Miss Africa 2016, imeanzishwa mwaka huu, kwahiyo haya ni mashindano ya kwanza. Mashindano haya ya Miss Africa 2016 yamebeba kauli mbiu "green economy, a tool for sustainable development" yaani Uchumi unaozingatia, kutunza n.a. kujali mazingira. Kwahiyo mashindano ya Miss Africa 2016 yanatafuta mrembo ambaye atatangaza na kuwakilisha utunzaji wa mazingira na maendeleo endelevu. Nitahamasisha na kusaidia wananchi kuelewa madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi ( climate change).

 Pia nitaitangaza Nchi yangu ya Tanzania nje ya Nchi n.a. kimataifa na kuungana na taasisi mbalimbali kusaidia na kutafuta suluhisho na kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi. Mfano wa mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaleta wasiwasi sana ni kama tatizo la mlima wa kilimanjaro. Mlima unaotupa sifa za kila aina duniani na watu kuona uzuri wa nchi yetu. Kwa sasa mlima wetu upo hatarini na Kupoteza hadhi yake kutokana na barafu iliyopo katika mlima huo kuanza kuyeyuka kwa kasi ya ajabu ambayo imesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi. Utafiti wa wanasayansi unaonyesha kuwa kama Hali itaendelea kuwa hivi, barafu katika mlima kilimajaro inaweza kutoweka kabisa ifikapo mwaka 2025.


 Huu ni mfano unao onyesha jinsi mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kutuharibia mazingira na pia kutokua kiuchumi. Kuna mengi ambayo yanatukumba watanzania kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Huo mfano ni moja ya swala ambao nitaongelea sana nikiwa Nigeria. Kwahiyo, naenda kuwakilisha nchi yangu hasa kwenye suala zima la mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na vitu mbalimbali kama ukataji miti ovyo na uvuvi usio wa kitalaamu unaotukumba. Nimefurahi kwamba watanzania mwaka huu tumesisitiza na kutekeleza sana upandaji wa miti. #mtiwangu Nawahaidi kuwa balozi mzuri kwenye hili swala. Na nita post kila siku kujulisha events zinazoendelea Miss Africa 2016. Naomba tushirikiane sababu ninaenda kubeba na kuitangaza nchi.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment