Sababu kubwa ya Wasanii kushindwa kuingia kwenye tuzo za EATV Awards 2016 ni kukosa baadhi ya Vigezo ,Ingia nikujuze zaidiWasanii wengi wakongwe wamejikuta wako nje ya kinyanganyiro cha tuzo za EATV kufuatia kushindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa na waandaaji wa tuzo hizo, zinazifanyika kwa mara ya kwanza nchini kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Taifa.
Akiongea na waandishi wiki hii Mratibu wa tuzo hizo ambaye pia ni Mkuu wa masoko wa EATV, Roy Mbowe amesema wasanii wengi wenye majina, mara baada ya kusikia tangazo la kujisajili walikaa kimya wakitegemea kazi zao nzuri labda zitaingia bila kufuata vigezo.
“Wapo ambao waliwahi kuja na kujaza fomu lakini nao pia tulipoenda BASATA tutakuta kwamba hawajajisajili kama wasanii rasmi kwa hiyo wakakosa sifa za kushiriki tuzo hizi na kinyume na matarajio ya wengi, wasanii ambao hawana majina makubwa lakini wenye kazi bora wakajikuta wanatawala tuno” alifafanua Mbowe.
Majina ya wasanii 45 walioingia katika kinyang’anyiro hicho yalitajwa Ijumaa iliyopita ambapo namba kubwa ya wasanii si wenye majina makubwa hali iliyopelekea minong’ono miongoni mwa mashabiki ambao wamekuwa na hisia kwamba tunzo hizo huenda zikawa na upendeleo.
Jumla ya tuzo 10 zinatarajiwa kukabidhiwa kwa wasanii wa muziki na filamu nchini Desemba 10 katika ukumbi wa Mlimani City, shughuli iliyodhaminiwa na makampuni ya Coca Cola, Barclays Bank na Vodacom.
credit:Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment