Tunafunga vyuo vyote visivyo na sifa, hakuna mjadala -Serikali


Waziri wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako, amesema serikali itavifunga vyuo vyote vya elimu ya juu visivyo na sifa ili kuliwezesha taifa kuwa na wahitimu wenye kukuza uchumi wa nchi.
Waziri huyo ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la siku mbili la Vyuo vya Elimu ya Juu.
“Tuna vyuo ambavyo havina ubora vitafungwa hilo halina mjadala,hata wanafunzi walio katika hivyo vyuo kwasababu utaratibu wa sasa wanafunzi kuomba vyuo vikuu wanapita kwenye chombo chetu Tume ya vyuo vikuu Tanzania kwahiyo wale wanafunzi bado itakuwa ni jukumu la serikali kuangalia kwamba tunawapeleka wapi lakini hatma ya wanafunzi inategemeana na atakapopelekwa,”alisema Ndalichako.
“Kwa nfano nikitoa mfano wa chuo kikuu cha Saint Joseph kama mnakumbuka mwezi wa pili tulifunga vyuo vya Saint Joseph na wale wanafunzi walipoenda tulivyowatawanya ilionekana ujuzi na maarifa walionayo ni kiwango cha chini kabisa,”aliongeza.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment