Alikiba Apata tuzo ya Soka Best Celebrity Player huko Uganda

Msanii wa Bongofleva Alikiba Jumamosi ya December 17 2016 alikuwa Uganda kucheza mchezo wa Hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kusaidia wa mama wajawazito ambao unajulikana kama Dorah Foundation.

Alikiba akiwa katika mchezo huo wa soka wa hisani uliyowahusisha mastaa mbalimbali, upande wake wa The Celebrity White Team waliibuka na ushindi wa goli 4-1, huku Alikiba akiwa kahusika katika upatikanaji wa goli la pili katika ushindi huo.

Alikiba na Emanuel Okwi
Upande wa timu ya Alikiba alikuwa na staa wa soka aliyetamba na Simba na Yanga Emanuel Okwi, ambapo mchezo ulimalizika na Alikiba katika mchezo huo wa hisani alipewa tuzo ya The Best Celebrity Player Award, kama hufahamu ukiachana na muziki Alikiba pia ana uwezo wa kucheza mpira.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment